KATIBA :RASIMU YA KATIBA MPYA CHENGE AIWEKA HADHARANI KUPIGIWA KURA JUMATATU SEPT 29 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Sept 2014

KATIBA :RASIMU YA KATIBA MPYA CHENGE AIWEKA HADHARANI KUPIGIWA KURA JUMATATU SEPT 29



Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo, Andrew Chenge, bungeni mjini Dodoma, Jumatano Septemba 24, 2014 ambapo aliiweka hadharani rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayopendekezwa na bunge hilo, ambapo Jumatano Septemba 29, 2014 itapigiwa kura na wabunge hao imma kjuikubali au kuikataa. Endapo itapita basi hatua itakayofata kama Munghu akitujaalia, ni kupigiwa kura na wananchi ili kuihalalisha au kuikataa.
Chenge akiwasilisha rasimu hiyo

Mwenyekitin wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta, akiwaonyedsha wajumbe wa bunge hilo kijitabu cha rasimu ya katiba inayopendekezwa kabla ya kusomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo, Andrew Chenge

Chenge akiwasilisha rasimu hiyo mbele ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba bungeni mjini Dodoma

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar, akitafakari wakati rasimu hiyo ikisomwa

Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, waliochangia pakubwa haki za wasanii kutambuliwa kwenye katiba inayopendekezwa mmoja wao ni Martha Mlata amaye naye ni msanii wa nyimbo za injili

Waziri MkuuMstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanavikundi waliofika bungeni kusikiliza rasimu ya katiba inayopendekezwa

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda (Wapili kushoto), akiwa na baadhi ya wasanii wakiongozwa na rais wao, Saimon Mwakifwamba (Kulia)

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Martha Mlata (Wapili kushoto), akipiga picha na rais wa wasanii nchini Saimon Mwakifwamba (Kushoto) na msanii nguli Stara Thomas (Watatu kushoto) mara baada ya kusomwa rasimu hiyo. Mlata amechangia pakubwa kuhakikisha haki za wasanii zinatambuliwa kwenye rasimu hiyo

Rais wa wasanii nchini Saimon Mwakifwamba akimpongeza Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Martha Mlata . Picha na Khalfan Said

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad