MATUKIO YA MOTO : MHE. LOWASSA ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI AMBALO BWENI LAKE LILITEKETEA KWA MOTO, MONDULI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Jul 2014

MATUKIO YA MOTO : MHE. LOWASSA ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI AMBALO BWENI LAKE LILITEKETEA KWA MOTO, MONDULI ARUSHA


Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto (Jumatano) asubuhi.

Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.

Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kulifikisha wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa  ametembelea shule hiyo na kiahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati  utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.Gharama za kuwasafirisha ni shilingi laki Saba.

Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
 Zimamoto kutoka  Arusha mjini wakizima moto huo.
 Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.

Lowassa akikagua uharibifu huo wa mato.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad