Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo
wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni
yao kuteketea na moto (Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kulifikisha wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na kiahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.Gharama za kuwasafirisha ni shilingi laki Saba.
Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.

Zimamoto kutoka Arusha mjini wakizima moto huo.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa
afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea
mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli
yaliyoteketea kwa moto.
Lowassa akikagua uharibifu huo wa mato.
No comments:
Post a Comment