BOMU LALIPULIWA SOWETO ,JIJINI ARUSHA LAUA ZAIDI YA WATU WAWILI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Jun 2013

BOMU LALIPULIWA SOWETO ,JIJINI ARUSHA LAUA ZAIDI YA WATU WAWILI

Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu wa wawili na zaidi ya majeruhi 62 wameumia vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu. Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara baada tu ya Mh. Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda alilenga kuwajeruhi viongozi hao.

DSC07403
Lakini jambo la kushnagaza kidogo ni milio ya risasi za mto iliyofuatia mfululizo baada tu ya kishindo cha mlipuko wa bomu na hata baadhi ya majeruhi wameelezwa kukutwa na risasi mwilini na pia inadaiwa maganda kadhaa ya risasi yameokotwa viwanjani hapo. Blogu hii ilishuhudia mama mmoja akiwa na tundu kubwa kifuani linalodhaniwa kutokana na risasi ya mto. Haijaweza kufahamika waliofyatua risasi hizo ingawa askari Polisi walikuwepo wengi na wengine wakivalia kiraia.

Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa kwanza baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa, na hivyo baadhi kuhamishiwa hopsitali nyingine kama Seliana na AICC kwa matibabu ya haraka.

Baadhi ya majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wa Arusha, sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo watoto waliofika mkutanoni hapo.

Mkutano huo ulivunja rekodi ya mahudhurio viwanjani hapo.. lakini ulikuja kuharibika baada ya kutokea mlipuko huo haotuba zikiwa zimeishamalizika na baadhi ya watu wakiwa wanatawanyika kuelekea majumbani huku zoezi la kuchangisha pesa likiendelea, kitendo kilichowazuia hata wakusanyaji michango kushindwa kumalizia zoezi hilo…

Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na baadae kukimbilia nyumba zilizojirani.

Mbowe - SowetoMwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha,katika Mkutano wa Chadema kufunga kampeni zake.
DSC07401Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
DSC07413Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya
DSC07407Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini
DSC07408
DSC07426Mama huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja inadaiwa amejeruhiwa na risasi kifuani kama jeraha linavyoonesha, akiwa anahema kwa shida akiwahishwa hopsitalini. Kwa hisani ya Arusha 255 Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad