UKAGUZI WA UJENZI WA WODI ZA WAGONJWA WA FISTULA CCBRT WAFANYIKA. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Nov 2012

UKAGUZI WA UJENZI WA WODI ZA WAGONJWA WA FISTULA CCBRT WAFANYIKA.


 Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, akipokea zawadi kutoka kwa moja ya wagonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT wakati alipofanya ukaguzi wa wodi mpya za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Rais. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja nae ni Mkurugenzi  wa Idara ya huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet. 
 Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi Kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Ujenzi wa Hospitali Tom Bourel wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Dk. Jakaya Kikwete mapema Mwezi huu, Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Peter Slaa
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi Kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Ujenzi wa Hospitali Tom Bourel wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Dk. Jakaya Kikwete mapema Mwezi huu, Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Peter Slaa

Mkurugenzi  wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akikagua moja ya mabasi yatakayo tumika kubeba wagonjwa wa Fistula, mabasi hayo yamenunuliwa katika mpango wa kupambana na Fistula uliochini ya CCBRT, Wizara ya Afya na Vodafone uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Februali 25.



Ukaguzi wa Ujenzi  wodi za wagonjwa wa Fistula CCBRT wafanyika.
*    Tayari kukabidhiwa kwa Mh.Rais Dk. Jakaya Kikwete.
*    Idadi ya wanawake wanaofanyiwa upasuaji yaongezeka.

Dar es Salaam, 13 Novemba 2012 ... Mkurugenzi wa Idara ya tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando na Mkurugenzi wa huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnett pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya CCBRT Dr. Wilbroad Slaa, jana wamefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula pamoja na mabasi matatu ya kubeba wagonjwa katika hospitali ya walemavu ya CCBRT kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete hivi karibuni. 

Septemba mwaka 2011, CCBRT na Vodafone Foundation pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, waliungana kwa pamoja katika kupambana na magonjwa mbalimbali ya uzazi kwa wanawake ukiwemo ugonjwa wa fistula ambao umekuwa tishio kwa kinamama wengi hapa nchini. Kampeni hiyo iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete tarehe 25 ya mwezi Februali na kuwezesha upatikanaji wa Dola za kimarekani milioni 10.

Baada ya huduma ya Vodacom M - pesa kuanza kutumika kutuma fedha za usafiri na matibabu kwa wagonjwa wa Fistula walioko katika maeneo ya vijijini, kuja CCBRT ili kupata matibabu mpango huo umeiwezesha hospitali hiyo kutoa matibabu kwa wagonjwa wapatao 1000.

Akizungumzia mpango huo Dr. Janis Perialis ambaye ni mtaalam wa upasuaji wa ugonjwa wa Fistula amesema kuwa mpango wa kusafirisha wagonjwa kwa kuwatumia fedha kupitia M - pesa umewezesha hospitali hiyo kupambana na Ugonjwa wa Fistula kwa kuwafikia wanawake wengi zaidi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.

"Tunao mabalozi wetu katika mikoa mbalimbali nchini, wanapopata taarifa kuhusu mwanamke mwenye fistula wanatupa taarifa na pesa inatumwa kupitia M pesa na wagonjwa wanapofika Dar es salaam hupokelewa na kuletwa katika hospitali yetu, mpango huo umetuwezesha kupokea wagonjwa kutoka katika mikoa tofauti nchini na kuwafanyia upasuaji na hatimaye kuwarudisha kwao wakiwa salama" alisema Perialis.

Mwaka 2014, CCBRT itafungua hospitali mpya ya huduma za  uzazi na watoto itakayotumika kama rufaa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na kupanua huduma zake kanda ya mashariki, ili kutoa huduma za uzazi na pia itatumika kama kituo cha mafunzo kwa wataalam wa afya nchini. 

"Mchango wa Vodafone Foundation tayari umeleta mabadiliko makubwa katika kupambana na ugonjwa wa fistula nchini Tanzania. Mafanikio haya yasingefikiwa bila ya mchango mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Ally Mwinyi," alisema Erwin Telemans, Mkurugenzi wa CCBRT.
"CCBRT inatumia teknolojia ya simu kupitia huduma ya M - pesa kufanya malipo kwa ajili ya usafiri wa wagonjwa wenye Fistula katika maeneo ya vijijini nchini. Vodafone Foundation inajivunia kufanya kazi na CCBRT katika kuboresha huduma za uzazi nchini, "Kwa pamoja tutabadilisha maisha ya wanawake wengi duniani," alisema Andrew Dunnett, Mkurugenzi wa huduma za jamii wa Vodafone group.
Kwa Wahariri:

Kazi ya CCBRT katika kupambana na Fistula.
*    Ugonjwa wa Fistula husababishwa na maumivu ya muda mrefu wakati wa uja uzito bila kupata matibabu. Madhara ya fistula ni ya muda mrefu, husababisha motto kufa na mwanamke kuendelea kutokwa na haja mfurulizo.
*    Hospitali ya CCBRT ni pekee inayotoa matibabu kwa wagonjwa wa Fistula Tanzania.
*    CCBRT inatoa matibabu kwa wagonjwa wa Fistula Bure.
*    CCBRT inatumia teknolojia ya simu ya Vodafone, M - Pesa kulipia huduma za usafiri kwa wagonjwa, na hivyo kuhakikisha wanawake wasiojiweza waishio katika maeneo ya vijijini wakipata matibabu.
*    Kwa mwaka huu CCBRT imetibu wanawake 400 wenye ugonjwa wa Fistula.

Kuhusu Vodacom Tanzania:
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na  jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.  Vodacom Foundation  ina nguzo kuu tatu: Afya,  Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi  sasa taasisi hiyo  imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha,  imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa  na kampuni mama ya Vodafone  .  
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia  teknolojia ya kisasa  ya  mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki  hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na  asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa  Super Brand (Chapa Bora Zaidi)  kwa miaka  mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad