TAARIFA KWA UMMA
Uzinduzi wa Shindano la kusaka Mabingwa wa Kero kwa Wateja
Jumuiya ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya
Facebook na Twitter wamezindua rasmi shindano la kusaka kampuni inayotoa huduma
na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.
Jumuiya
hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati,
waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, viongozi wa makampuni mbalimbali
nchini na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.
Lengo
la
jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara au watoa huduma mbalimbali
nchini kutoa huduma bora kwa wananchi haswa ikizingatiwa wateja hawa
hutumia fedha zao kulipia huduma na bidhaa hizo . Kauli mbiu ya
wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme.
Katika
wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa
katika shindano hilo kwa kulalamikiwa na wateja wao. Kwa taarifa zaidi kuhusu
ni kampuni zipi zinashikilia usukani fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook
linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili
kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai ya Twitter au ya Facebook
na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utakuwa
umeifanya kampuni ulioitaja kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa
huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma
Bongo
inatoa wito kwa wakazi wa Arusha ambao kero zao zimeshindwa kutafutiwa
ufumbuzi kushiriki kwa wingi katika shindao hilo ili kukomesha tabia
hizi zinazorudisha maendeleo nyuma maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment