Na Mwandishi Wetu , Dar.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeahidi kufanyakazi na Mtandao wa Wana Blogu Tanzania (TBN), pamoja na vyama vingine vya waandishi wa habari ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Injinia Andrew Kisaka, alipokutana na ujumbe wa TBN ofisini kwake, katika kikao cha kujadiliana mambo mbalimbali zikiwamo changamoto zinazowakabili bloga nchini.

"Sisi huwa tunapenda kufanya kazi na vyama ambavyo vinawakilisha mahitaji na matakwa ya wanachama wao, badala ya kufanyakazi na mwaandishi mmoja mmoja...tunafurahi sana kufanyakazi na waandishi kupitia vyama vyao," alisema Injinia Kisaka.

Injinia Kisaka amesema kuwa TCRA imefurahi kukutana na TBN kwa kuwa wanafahamu kuwa bloga wanasehemu kubwa sana kwenye maudhui ya ndani, na hata kwenye usajili wa TCRA bloga wanachukua nafasi kubwa sana katika maudhui ya mtandaoni.

"Kwa hiyo TBN mtakuwa silaha moja wapo nzuri sana yakutuwezesha sisi kama Mamlaka ya Mawasiliano nchini, tunao simamia utangazaji pamoja na maudhui ya mtandaoni kuwa karibu na nyinyi na kuhakikisha maudhui ya mtandaoni yanaleta tija na maendeleo kwa wananchi," alisema Injinia Kisaka
1000247590 
Viongozi waliokutana na Mhandisi  Andrew Kisaka  uliongozwa na Katibu Mtendaji wa TBN Khadija Kalili ,Kaimu Mwenyekiti TBN Rwehabura Rugambwa   ,Mweka Hazina Beda Msimbe  na Wajumbe  Muhidin Issa Michuzi, Frank Wandiba, Carren Mgonja na Shaaban Lulela . 
Mamlaka ya wasiliano Tanzania (TCRA) leo tarehe 19.03.2025 imekutana na na Uongozi wa Tanzania Bloggers Netwark (TBN) katika Ofisi za TCRA Makao Makuu Jijini Dar Es Salaam.


Katika kikao hicho TBN imeiomba TCRA kupunguza gharama za usajili wa Blogu kama siuo kuziondoa kabisa.

Aidha TBN imeiomba TCRA iwe inatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa Bloggers ilikuwajengea uzoefu katika kazi zao za kila siku.

Baada ya kusikiliza maombi hayo  Meneja wa Huduma za Utangazaji  TCRA Mhandisi Andrew Kisaka amesema wameyapokea maombi ya TBN na watayafanyia kazi huku ameahidi kutoa mrejesho.

Mhandisi  Kisaka ambaye ndiye alikua mwenyeji wa msafara huo wa Viongozi  wa TBN  amesema kuwa kwa niaba ya TCRA,

1000247591
Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua jambo mbele ya kamati ya Uongozi TBN iliyofika ofisini kwake leo  tarehe 19.Machi.2025 Jijini Dar es Salaam. 
1000247595
 "Tunafurahi kukutana nanyi leo na kujadiliana mambo mbalimbali sambamba na kutambua namna mnavyoendesha shughuli za kihabari maana Bloggers mna umuhimu mkubwa sana kwenye maudhui ya ndani na kwa mustakabali wa nchi kwa ujumla hivyo ninawaahidi kuwa tumepokea maombi yenu, tutayanyia kazi na majibu tutawapatia" amesema Mhandisi Kisaka.