Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano Septemba 4,2024 yaliyofanyika kwenye Kikosi cha 832KJ,Ruvu kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi .
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Oparesheni miaka 60 ya Muungano wengine walioketi ni Maafisa na viongozi waliofika kwenye sherehe hizo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Solitina Bernad Nshushi
Mwakilishi wa mkuu wa JKT, Kanali George Barongo akitoa salam kwenye sherehe ya kufunga mafunzo ya vijana kwa mujibu wa sheria Operesheni miaka 60 ya Muungano.
Wahitimu wa mafunzo ya mujibu wa sheria Oparesheni miaka 60 ya JWTZ, Kikosi 832 KJ Ruvu kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani
Kamanda wa Kikosi 832 KJ Ruvu Kanali Peter Elius Mnyani akizungumza kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya vijana wa mujibu wa sheria Oparesheni miaka 60 ya Muungano ,yaliyofanyika leo Septemba 4,2024 Mlandizi Mkoani Pwani.
Na Khadija Kalili , Michuzi Tv
VIJANA wahitimu wa mafunzo ya kwa mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano ya kikosi namba 832 KJ Ruvu wameahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga uchumi imara kwa maslahi ya taifa kutokana na mafunzo ya jeshi la awali waliyopata.
Akisoma risala kwa niaba ya Wahitimu wa mafunzo ya Vijana wa Mujibu wa Sheria operasheni miaka 60 ya Muungano 832 KJ Ruvu Hilda Edward amesema kutokana na mafunzo ya wiki 12 waliyopata kujifunza utii, Uzalendo, uadilifu na kuchapa kazi.
wameahidi kuzingatia mafunzo yote kwa kuhakikisha rasimali za nchi yetu hazipotei wakizingatia mafunzo waliyopatiwa katika kipindi chao cha mafunzo.
"Tunaahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga uchumi imara kwa maslahi mapana ya nchi yetu" amesema Hilda.
Amesema yeye na wenzake wanatoa ahadi kwa Dkt. Samia kwamba watadumisha uzalendo, utii nidhamu uaminifu na kwa taifa.
Aidha Wahitimu hao kwa pamoja wamekula kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu na kutoa shukrani za pekee kwa Wakufunzi wao kwa kuwapatia stadi za maisha katika kipindi chote cha miezi mitatu walipokuwa Kikosini hapo.
Vijana hao ambao wametoka katika maeneo mbalimbali wamejifunza ukakamavu, kilimo na ufugaji, usanii na michezo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Solitina Bernad Nshushi amesema kuwa anawapongeza vijana wote kwa kukubali kuja kujifunza mafunzo haya ya kwa mujibu wa sheria kwa sababu kwa kufanya hivyo wamejitende haki wenye na katika jamii waliyotoka na taifa kwa ujumla.
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali George Barongo Kazahura amesema mafunzo haya mliyoyapata sasa mmefahamu dhana ya uzalendo mmekua tayari kutumikia taifa popote mtakapokuwa hivyo basi mnapaswa mkatumie elimu hiyo pasipokuvunja utaratibu na sheria za nchi.
Kamanda Kikosi cha 832 Ruvu JKT Kanali Peter Elius Mnyani amesema vijana waliohitimu mafunzo yao leo Septemba 4,2024 stadi za maisha elimu hii waliyoipata imewajenga kifikra mbalimbali za ulinzi na usalama na wamekidhi vigezo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa vijana wetu ambao mmehitimu mafunzo ya kwa mujibu wa sheria leo nendeni mkatumie fursa mbalimbali ambazo mmepatiwa.
"Kama jinsi Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alivyosema katika maadhimisho ya miaka 69 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwa nchi yetu iko salama vivo hivyo sina budi kusema kuwa kweli hakuna shaka nchi yetu iko salama kiulinzi na usalama kichumi pamoja na huduma za kijamii, JKT ni tanuri linalofunda vijana kuwa wazalendo kwani hata ninapowaangalia naiona Tanzania inayoongoza kiuchumi na vijana wanaotumia
fursa bila kulalamika hivyo katumieni mbinu za mafunzo mlizopata katika hapa Kambini na mkawe mabalozi wema kwa vijana wengine.
No comments:
Post a Comment