Lengo ni kuboresha usalama barabarani kwa waendesha pikipiki jijini Dar es Salaam
Tanzania Breweries Limited (TBL), kwa kushirikiana na Tanzania Red Cross Society (TRCS), inajivunia kutangaza uzinduzi wa Mpango wa Mafunzo na Elimu kwa Waendesha Pikipiki. Mradi huu utaendeshwa kuanzia Septemba hadi Desemba 2024 na unalenga kupunguza ajali za barabarani zinazohusisha waendesha pikipiki kupitia programu ya kina ya elimu na mafunzo inayolenga kuimarisha uelewa, kuboresha ujuzi wa uendeshaji, na kukuza mazoea salama ya kuendesha pikipiki.
Waendesha pikipiki wanaotoa huduma za usafiri jijini Dar es Salaam watakuwa walengwa wakuu wa mpango huu. Waendesha pikipiki hawa watafikiwa kupitia vyama vyao vilivyopo kwenye wilaya nne za Dar es Salaam: Kinondoni, Ubungo, Ilala, na Temeke.
Mpango huu utabuni na kutekeleza mtaala maalum, kuanzisha ushirikiano wa kimkakati na shule za uendeshaji, kushirikisha jamii kupitia warsha, na kuendesha kampeni za uhamasishaji.
Zaidi ya hayo, mradi unalenga kuongeza uelewa kuhusu huduma za kwanza miongoni mwa vyama vya waendesha pikipiki na kuanzisha jamii za waendesha pikipiki zitakazosaidia kutoa huduma za kwanza kwa wahanga wa ajali.
Malengo ya programu ni pamoja na:-
* Kuongeza uelewa: Kuimarisha uelewa wa waendesha pikipiki kuhusu sheria za usalama barabarani na mazoea salama ya kuendesha kwa 50% ndani ya mwaka wa kwanza.
* Kupunguza ajali: Kupunguza ajali na vifo vinavyohusisha pikipiki kwa 30% ndani ya miaka mitatu.
* Kushirikisha waendesha pikipiki: Kuwashirikisha angalau waendesha pikipiki 10,000 nchini Tanzania katika mpango wa mafunzo ndani ya miaka miwili ya kwanza.
Ili kufikia malengo haya, mradi utashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo mamlaka za serikali za mitaa, vyama vya waendesha pikipiki, vikosi vya polisi (Kitengo cha Usalama Barabarani), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), na viongozi wa jamii. Shughuli zilizopangwa ni pamoja na: • Vikao vya utambulisho na mamlaka za serikali • Uorodheshaji wa wadau • Utafiti wa awali kutathmini uelewa wa sasa na uwezo wa waendesha pikipiki • Vikao vya wadau na uorodheshaji wa vikundi vya waendesha pikipiki • Mafunzo ya usalama barabarani na huduma ya kwanza kwa waendesha pikipiki • Ubunifu na uwekaji wa alama za usalama barabarani kwenye vituo vya waendesha pikipiki • Vikao na kampeni za uhamasishaji kupitia vyombo vya habari • Usambazaji wa vipeperushi vya usalama barabarani • Ziara za ufuatiliaji za kila mwezi na kila robo mwaka • Ununuzi na usambazaji wa vifaa vya huduma ya kwanza • Warsha ya mafunzo yaliyopatikana
Mradi utachukua njia ya ushirikishwaji, ukiweka jamii katikati ya hatua zote na kuhakikisha uratibu na ngazi mbalimbali za serikali, maafisa wa maendeleo ya jamii, na polisi. Mfumo wa maoni kutoka kwa jamii utatumiwa kukusanya maoni na kuhakikisha uwajibikaji.
Michelle Kilpin, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Breweries Limited, alisema, "Tanzania Breweries Limited inaunga mkono lengo la maendeleo endelevu ya umoja wa kimataifa (SDG) la kupunguza kwa nusu ya idadi ya vifo na majeraha yatokanayo na ajali za barabarani ifikapo 2030.

Tunaamini kampuni yetu ina fursa ya kipekee ya kuboresha usalama barabarani na kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu. Mpango huu wa usalama barabarani ni sehemu ya juhudi zetu za Kampeni ya Smart Drinking na kipaumbele kwetu kutokana na kwamba wenzetu, familia zao, na wateja wetu wanasafiri barabarani kila siku."
Reginald Mhango, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Shirika katika Tanzania Red Cross Society, alisisitiza umuhimu wa mpango huu: "Ongezeko la ajali zinazohusisha pikipiki nchini Tanzania linahitaji hatua za haraka. Mradi huu unalenga kushughulikia changamoto hizi kupitia elimu na mafunzo ya kina, hatimaye kupunguza vifo na majeraha."

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Michelle Kilpin, akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Elimu na Mafunzo kwa Waendesha Pikipiki uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo, ambao ni ushirikiano kati ya TBL na Tanzania RedCross Society(TRCS), unalenga kuboresha usalama wa waendesha pikipiki. Kulia ni Said Kagomba, Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Tanzania
No comments:
Post a Comment