Michezo : Wanamichezo wa Tanzania Wajiandaa kutupa Karat zao za Kwanza kwenye Michezo ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Monday, 29 July 2024

Michezo : Wanamichezo wa Tanzania Wajiandaa kutupa Karat zao za Kwanza kwenye Michezo ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024


WANAMICHEZO watatu wa Tanzania walioko Paris kwenye michezo ya 33 ya Olimpiki ya majira ya joto ya Paris 2024 wameendelea na mazoezi makali chini ya makocha wao, wakijiandaa kwa michuano yao inayoanza rasmi kesho Jumatatu Julai 29, 2028.

Tanzania itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano hii ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya joto kesho Jumatatu Julai 29, 2024 wakati mchezaji wake wa Judo, Andrew Thomas Mlugu, atakapopanda ulingoni kupambana na William Tai Tin, judoka wa kutoka nchi ya Samoa. Mpambano wao utakuwa saa 5 asubuhi kwa saa za Tanzania.

Tai Tin anatoka Siumu na Kisiwa cha Manono lakini anaishi Melbourne, Australia, na alikuwa sehemu ya timu ya Samoa katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2022 huko Birmingham. Ana umri miaka 39.

Siku ya pili, yaani Jumanne Julai 30, 2024 Tanzania itatupa karata yake ya pili wakati muogeleaji Collins Phillip Saliboko, atakapoingia bwawani kushindana katika mita 100 (Freestyle) kwa wanaume mnamo saa 6:15 mchana kwa saa za Tanzania.

Karata ya tatu ya Tanzania itatupwa Jumamosi Agosti 3, 2024 na mwogeleaji Sophia Anisa Latiff ambaye atashindana katika mita 50 (Freestyle) kwa wanawake mnamo saa 6:00 mchana kwa saa za Tanzania.

Andrew Thomas Mlugu - Judo

*Tarehe ya Kuzaliwa: Novemba 12, 1995


*Mahali pa Kuzaliwa: Kinondoni, Tanzania


*Jinsia: Mwanaume


*Uzito: 73 kg


*Urefu: 158 cm

*Kushindana Jumatatu Agosti 29, 2024 (Saa 5 Asubuhi, kwa saa za Tanzania)


Andrew Thomas Mlugu ni Judoka maarufu nchini akiwa muajiriwa wa Jeshi la Magereza.

Akiwa na urefu wa sentimita 158 na uzito wa kilo 73, Andrew anashindana katika daraja la uzito wa kilo 73 kwa wanaume. Mafanikio yake makubwa ni pamoja na kushiriki katika Olimpiki ya Majira ya Joto ya 2016, ambapo aliwakilisha Tanzania na kuonyesha ujuzi wake wa judo kwenye moja ya majukwaa makubwa zaidi duniani.


Akiwa mmoja wa wabeba bendera wa Tanzania wakati wa Gwaride la Mataifa katika Ufunguzi rasmi Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Andrew sio tu alishindana, bali pia juhudu zake ujitolea kwenye judo kunaendelea kuhamasisha wanamichezo wengi wachanga nchini Tanzania.


Andrew amekuwa mchezaji mwenye bahati baada ya kuchaguliwa kujiunga na kambi maalumu ya maandalizi kwa michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 na kufanya mafunzo na mazoezi kwa muda wa mwaka mmoja nchini Ufaransa.


Collins Phillip Saliboko - Kuogelea

*Tarehe ya Kuzaliwa: Aprili 9, 2002


*Mahali pa Kuzaliwa: Mbeya, Tanzania


*Jinsia: Mwanaume


*Uzito: 72 kg


*Urefu: 168 cm

*Kiushindana; Julai 30, 2024 (Saa 6:15 mchana, kwa saa za Tanzania)



Collins Phillip Saliboko ni nyota inayochipukia katika kuogelea nchini Tanzania.

Kijana huyu mzaliwa wa Mbeya, ni muogeleaji aliyeonesha ustadi mkubwa katika bwawa la kuogelea.


Akiwa na urefu wa sentimita 168 na uzito wa kilo 72, Collins ana sifa za kimwili zinazokamilisha ujuzi na kasi yake.


Kujitolea kwake kwenye mchezo kumemfanya kushiriki katika mashindano mengi ya kimataifa, akiwakilisha Tanzania kwa Fahari, ikiwa ni ud awa wa kazi yake ngumu na jitahada alizonazo katika michezo ya kuogelea nchini Tanzania.


Collins ameshiriki mashindano yafuatayo;

Men 50m (Freestyle) World Aquatic Championship Tokyo, Japan, 2023 akishika nafasi ya 21 kwa kutumia mud awa dakika 24:44


Men 200m (Butterfly) Commomnwealth Games Birmingham, UK, 2022, akishika nafasi ya 10 kwa kutumia muda wa dakika 2:23.25


Men 50m (Freestyle) CANA Zone IV Swimming Championship 2022, Lusaka, Zambia, akishika nafasi ya 20 kwa kutumia mud awa dakika 1:04:43


Men 200 (Butterfly) 14th CANA African Senior Swimming and Open Water Championship 2021, Accra, Ghana, akishika nafasi ya 19 kwa kutumia ud awa dakika 02:13:39


NB: Kirefu cha CANA ni Confederation Africaine de Nation (African Swimming Confederation) ambayo sasa inaitwa Africa Aquatics. Ni Shirikisho la bara la Africa linalosimamia michezo yote ya majini. Lilianzishwa mwaka 1970 na wanachama 7. Kufikia mwaka 2008 limekuwa na wanachama 43, Tanzania wakiwa mojawapo.



Sophia Anisa Latiff – Kuogelea

*Tarehe ya Kuzaliwa: Desemba 24, 2006


*Mahali pa Kuzaliwa: Uingereza


*Jinsia: Mwanamke
Uzito: 60 kg


*Urefu: 161 cm

*Kushindana; Agosti3, 2024 (Saa 6:00 mchana, kwa saa za Tanzania)


Sophia Anisa Latiff, ambaye alizaliwa nchini Uingereza, ni muogeleaji mchanga na mwenye matumaini kubwa ya kuiwakilisha Tanzania kwa muda mrefu siku za usoni.


Akiwa na urefu wa sentimita 161 na uzito wa kilo 60, Sophia anachanganya wepesi na uvumilivu, sifa muhimu kwa kuogelea kwa ushindani. Licha ya umri wake mdogo, tayari amejiwekea jina katika jamii ya kuogelea.


Historia yake, akiwa amezaliwa Uingereza, inaongeza kipengele cha kipekee cha uzoefu na mwonekano wa kimataifa kwenye kuogelea kwa Tanzania. Talanta na uwezo wa Sophia vinamfanya kuwa mtu wa kuangaliwa katika kuogelea.

Sophia ameshiriki mashindano yafuatayo
Women 100m (Breastroke) 14th CANA African Junior Swimming and open water Championship 2021, Accra, Ghana akishika nafasi ya 14 katika mud awa dakika 01:44:43

Women 100m (Freestyle) World Swimming Championship 2022, Melbourne, Australia akishika nafasi ya 15 katika muda wa wa dakika 01:44:43

Women 50m (Freestyle) World Aquatic Junior Championship 2023, Netanya, Israel, akishika nafasi ya 16 katika mud awa sekunde 28:07

Karata nne za mwisho za Tanzania zitatupwa na wakimbiaji Marathon, ambao watawasili Agosti 7, wakitokea kambini Arusha moja kwa moja, tayari kwa mbio hizo zitazokuwa Agosti 10 na Agosti 11, 2024.

Safari hii mfumo wa michuano ya Marathon umebadilishwa, ambapo tofauti na ilivyozoeleka, wanaume ndio wataanza kukimbia na wanawake ndiyo watamalizia.

Hivyo basi, wakimbiaji wa Marathon kwa wanaume, yaani nahodha Alphonce Felix Simbu - nahodha na Gabrield Gerald Geay watashindana mnamo Agosti 10, 2024

Wakimbiaji wa Tanzania wa Marathon kwa wanawake, Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri wamepangwa kukimbia Agosti 11, 2024, ambayo ndiyo siku ya mwisho ya Paris 2024 Olympics.

No comments:

Post a Comment