Sheria : Waziri Ndumbaro atoa siku 30 Mawakili kutumia mihuri ya Kielektroniki - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 28 May 2022

Sheria : Waziri Ndumbaro atoa siku 30 Mawakili kutumia mihuri ya Kielektroniki


Na.Vero Ignatus, Arusha

Waziri wa Katiba na Sheria Damasi Ndumbaro ameagiza chama Cha mawakili (TLS)ndani ya siku 30 mawakili wote wawe na mihuri ya kieletroniki baada ya hapo Serikali haitambua mihuri ambayo siyo ya kieletroniki.

Ameyasema hayo katika mkutano wa mwaka wa TLS Jijini Arusha kwamba Wizara itaandikia Mamlaka zote mabazo zinatambua mihuri ya Mawakili ikiwemo TRA, Mahakama na wadau wengine ya wasitambue muhuri mingine ambao siyo wa kieletroniki

"Tutaandikia Mamlaka nyingine zinazotambua mihuri ya mawakili kwmaba isitambue mihuri mingine Kama siyo ya kieletroniki"alisema Ndumbaro.

Dkt.Ndumbaro ameitaka TLS kuweka mikakati ya kukua zaidi siyo kiidadi bali kimfumo kiuendeshaji kitaswira na na muhimu zaidi kiuchumi,kutokana na kaulimbiu ya mwaka huu inayosisitiza kukua zaidi huku akisema wanahitaji zaidi ukuaji huo uendane na kumnufaisha mwanachama haswa maawakili vijana.

Amewataka TLS kutimiza jukumu la kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamiii huku akirejea mazungumzo waliyofanya na Rais wa TLS Edward Hosea na sekretarieti kwamba wiki ya msaada wa kisheria isiwe inafanyika Mara moja kwa wiki kila Mwaka bali iwe endelevu

"Naomba nikwambie mhe.Rais tulilipokea hilo na tumeanza kulifanyia kazi Kama mmeona nilikuwa ana Balozi wa Ujeruman Juzi dar na katika mambo tulivyokubaliana liwatasaidia suala zima la ushauri wa kisheria' alisema Ndumbaro

Aidha Ndumbaro amesema kuwa kwa Mika mingi Kumekuwa na malalamiko ya watu kunifanya wakili na kutumia mihuri jambo ambalo TLS imekuja na ufumbuzi wa jambo hilo kwa kuandaa mihuri ya kieletroniki itakayokwenda kuondoka changamoto hiyo.

Amewataka mawakili hao kuzingatia maadili yao kazini kwa kutoa kwanza boriti kwenye macho yao,ili waweze kuona kibanzi kwenye macho ya wengine,na kuangalia jinsi gani wanaweza kufanya chaguzi mikutano mingine kwa kutumia teknolojia iliyopo sasakwani idadi ya mawakili imekuwa kubwa na siyo wote wanaweza kuhudhuria mikutano kwa wakati mmoja

"Pia tuangalie muda wa Uongozi kukaa mafarakani je kwa mwaka mmoja Uongozi unaweza kupanga na kufanikiwa?tuangalie pia gharama za kufanya uchanguzi kwa kujifunza nchi za wenzetu,pia tuangalie Nini nafasi ya mawakili nchini Tanzania abirtishen center

Aidha Waziri Dkt.Ndumbaro amewataka TLS kuondoa tofauti iliyopo Kati yao na Serikali kwani jukumu mmoja wapo walililonalo ni kuishauri Serikali siyo kuonyesha Kama wanaidhalilisha

"Unapompa mtu ushauri zipo njia mbalimbali hivyo ni Rai yangu kwamba tuangalie the best way ya kuishauri Serikali na siyo imefedheheswa kwani ndiyo huvuruga mahusiano Sasa ni vizuri tujitafajatri sisi wenyewe, turekebishe mambo yetu ya ndani na kuipitia sheria ya mawakili,pamoja na TLS sheria ili tuweze kusaidia wengine".Alisema Dkt.Ndumbaro.

Amewa kuwa Yale yote waliyokubaliana na wanachama wa Tanganyika law society watayatekeleza huku akitaja chama hicho kuwa ni Cha kitaaluma Cha zamani 54 ikiwa na wanachama 1000
Tunayo kila sababu ya kujipongeza kwa kukua kwa Kasi na idadi

Kw aupande wake Rais msataafu wa TLS John Seka amesema kuwa mambo ambayo wamefanikiwa kufanya siku ya leo ni kuzindua mfumo wa mihuri ya kieletroniki ambayo inatarajiwa kuwapa tija haswa kutokana na mawakili vishoka

"Kumekuwa na tatizo la mawakili wengi vishoka mihuri feki na kuwagongea watu nyaraka na kuwa changamoto kubwa mahakamani kwani Kumekuwa na watu waliopoteza haki zao za msingi

Akizungumzia uchaguzi wa kesho wa kumpata Rais mpya Seka alisema kuna changamoto kwani kuna ushindani mkubwa hivyo wanatarajia kusikia sera kwa Mara ya Mwisho na kuwatambua watu kwa kile watakachoifanyia TLS

Nae wakili Breati Kivea amesema kuwa Mhe.Waziri amewapa dawa kwani Mawakili wengi vijana walikuwa wanawategemea wateja ambao wanapatikana kwa njia za mihuri hivyo, Kumekuwa na ongezeko la watu kutumia mihuri ya mawakili kwa matumizi mabaya, ambapo imepelekea hadi mawakili wengine kuingia kwenye changamoto za utatishaji wa fedha

"Tumeshuhudua mawakili wakaifikishwa mahakamani kwmaba muhuriwake umetumika vibaya bila hata yeye kujua"alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati c
Ya maadili chama Cha mawakili (TLS) Abraham Bendera amesema kuwa amesema kuwa TLS amejiongeza kuwatambua watu wasio waaminifu wanaotumia mihuri ya mawakili vibaya, kwani walichikujanacho kinatambua kila kitu na taarifa za mtumishi kwani itaonyesha kumbukumbu mihuri umegongwa lini na wapi.

"Abraham amesema leseni za mawakili ni mwaka mmoja inapokuwa imemalizika hajapata leseni mpya muhuri haufanyi kazi kwa maana hiyo unaweza akuwadhibiti wale ambao ni mawakili wa kweli Ila wanafanya kazi nje ya muda wao wa uwakili"alisema

Aidha amesema muhuri huo utaondoa vishoka wanaotumia mihuri bila woga ,itawathibitishia mawakili kipato Chao kwani muhuri wake hauwezi kugongwa bila kuthibitika ,mawakili kwenye Jamii wataonekana wanatimiza majukumu yao na mahakama au sehemu ya jamii itahakikisha muhuri huo wa wakili.



Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damasi Ndumbaro akizungumza katika mkutano mkuu wa wa chama Cha wanasheria katika Kituo Cha Kimataifa Cha AICC Jijini Arusha Leo 26/5/2022

Baadhi ya wanachama Cha mawakili TLS wakiwa katika mkutano wa mwaka wa chama hicho amabao unaambatana na uchaguzi hapo kesho tar 27/5/2022 w akumpata Rais wa chama hicho
aadhi ya wanachama Cha mawakili TLS wakiwa katika mkutano wa mwaka wa chama hicho amabao unaambatana na uchaguzi hapo kesho tar 27/5/2022 w akumpata Rais wa chama hicho

No comments:

Post a Comment