Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani Ridhwan Kikwete akiwa ameambata na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Hajat Mwanaasha Tumbo leo Julai 23,2021 wamefika katika Shule ya Sekondari Kiwangwa na kujionea athari zilizotokana na moto ulioteketeza bweni la wasichana shuleni hapo ambapo wameazimia kurejesha mazingira katika hali yake ya kawaida ili watoto waendelee na masomo.
"Nimefika eneo la Shule ya Sekondari ya Kiwangwa kushuhudia uharibifu uliotokana na Moto uliounguza Bweni la Wasichana shuleni hapo. Shuleni hapo nimekutana na Katibu Tawala wa Mkoa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo. Tumejipanga kudhibiti na kuhakikisha hali inarudi vizuri kimasomo"alisema Mbunge wa Chalinze, Kikwete.
Bweni la wasichana Shule ya Sekondari Kiwangwa, lilishika moto na kuteketea kabisa usiku wa kuamkia leo Julai 23,2021 na hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.
Jengo la Bweni lililivyoteketea
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza na uongozi wa shule na mkoa
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza na uongozi wa shule na mkoa
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akitembezwa.
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo (mwenye babibui nyeusi) akizungumza.
No comments:
Post a Comment