Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Tanga Uwasa CPA Hussein
Ubbena akizungumza wakati wa mkutano huo |
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha
Mayala akizungumza wakati wa kikao hicho |
MKUTANO wa Wadau wa Tanga Uwasa kwa ajili ya kupata maoni kuhusu mkataba wa huduma kwa mteja ambao umefanyiwa marejeo mwaka 2021 umefanyika leo Jijini Tanga kwa kuwashirikisha Madiwani wa viti Maalumu,Maafisa Tarafa wa Jiji la Tanga na Maafisa Watendaji wa Kata.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema wameamua kukutana na viongozi hao kwa sababu wana watu wengi ambao wanawawakilisha na maoni yao ni kwa ajili ya wananchi wote na sio yao tu.
Alisema kwa sababu wao ndio viongozi waliopo kwenye maeneo hayo hivyo wajitahidi kuhakikisha ushiriki wao kwenye mkutano huo unakuwa na tija kubwa na sio bora mambo yaende hivyo hakikisheni mnatumia vizuri uwepo wenu.
“Tunazungumzia mkataba wa huduma kwa mteja amesema mwenyekiti hapa ni utawala bora lazima mnapokuwa mnapeana huduma muwe na kitu ambacho kinawaunganisha na kitu kinatuunganisha ni huu mkataba haki na wajibu wa pande zote mbili mtoa huduma na mpokeaji wa huduma “Alisema
Alisema wawasilishaji wa mada watawapitisha ili iwe rahisi kwenu kueleza muundo wa mkataba upoje?haki na wajibu upoje,zawadi na adhabu zipoje na mwisho wa siku ukikiuka mkataba tunakufanyaje hayo mambo yote inabidi tuyajadili kwa pamoja leo hapa“Alisema
Aidha alisema huo mkataba ni kwa wale watu ambao wana huduma na wale ambao bado hawana maana mwisho wa siku wataomba kwa ajili ya kuunganishiwa maji kwa sababu kuna vitu ambavyo anapaswa kufanya yeye na mtoa huduma na ukishafahamu hivyo itakuwa rahisi.
“Hiki ni kikao cha wadau tunakaa kwa ajili ya kupitia kwa sababu ni zoezi shirikishi na watakapomaliza hapo wataenda kukutana na wadau wengine halafu baada ya maoni yao yakishafanyiwa kazi yatapelekwa kwa mdhibiti Ewura kwa ajili ya kupitishwa rasmi na baadae watatengeneza vitabu watavigawa kwa wadau wao kwenye ofisi mbalimbali ikiwemo za Kata na watatoa nakala za kutosha ili kila mmoja aweze kupata.
Awali akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga Saumu Bendera alisema madhubuti ya mkutano huo ni kupitia maboresho ya mkataba kwa wateja .
Alisema kama wanavyojua maboresho mkataba ni kwamba mteja kuna haki na wajibu na pia vilevile mtoa huduma hivyo ni jambo jema ambalo linawapa wigo mpaka wa kutambua mambo mbalimbali.
Alisema kama wanavyojua Serikali imekuwa ikifanya maboresho ya kila siku na huo maana yake ni utawala bora kwa hiyo wamefika kama wadau kuweza kusikiliza maboresho hayo na wao wajue haki zao na wajibu wao na pia mtoa huduma na baadae watapitia na kuchangia.
Naye kwa upande wake,Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akizungumza katika mkutano huo wakati akiwasilisha mada ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Tanga Uwasa.
Alisema kwamba mkataba wa huduma kwa mteja unatakiwa kufanyiwa maboresho kila baada ya miaka mitatu na maboresho hayo yanapofanyika lazima wadau wahusishwe kuhusiana na nini ambacho kinajiri.
Alisema watawapitisha kwenye mkataba wote ili wapate kufahamu na kuona huo mkataba umehusisha nini na nini na maeneo gani ambayo yamefanyiwa maboresho.
Awali akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Haki na Wajibu wa Mteja Tanga Uwasa Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Tanga Uwasa CPA Hussein Ubbena alisema lengo la mkutano huo ni matakwa ya sheria kwamba serikali inataka Taasisi zake zote zinazotoa huduma ziwe zinaingia mikataba ya huduma bora na wateja wake hivyo leo walikuwa wanatimiza takwa hilo la kisheria.
Alisema kwamba Mamlaka iliandaa mkataba wao wa kutoa huduma na leo wamefanya wasilisho kwa wadau ambao ni watendaji wa serikali za mitaa na madiwani viti waliwasilisha mkataba ambao waliitengeza kama drafti ili waweze kupata maoni yao jinsi ya kuuboresha na hatimaye uweze kutumika.
No comments:
Post a Comment