Na Agnes Francis, Dar.
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30
katika kuelekea mwisho wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
ambao watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema
utaratibu huo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya
Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.
Ndimbo
amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki
wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora
kwa msimu huu.
Amewataja
wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis
Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce
Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na
Adam Salamba(Lipuli).
Wengine
ni Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya
(Singida), Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud
Ambokile(Mbeya City).
Pia
Shaaban Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga),
Gadiel Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey
Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John
Bocco(Simba), Jonas Mkude(Simba),
Erasto Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).
"Mchakato
wa kupata mchezaji bora unatarajia kufanyika Juni 23 mwaka huu katika
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ambapo msimu huu kutakuwa
na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet,"amefafanua
Pia
amesema licha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, kutatolewa tuzo
mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine
imeongezwa ikiwa ni katika uboreshaji
"Tuzo
iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili
kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala
ya kuwatenganisha, vile vilee msimu huu imeongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora
Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita.Hiyo ni kutokana na kuthamini
nafasi ya waamuzi wasaidizi,"amesema Ndimbo
Kwa
mazingira hayo tuzo zitakazotolewa siku hiyo ambapo wadhamini wakuu ni
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni Bingwa,Mshindi wa Pili,Mshindi
wa Tatu,Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora,Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi,Mwamuzi BoraKipa Bora,Kocha Bora,Goli Bora VPL,Best Eleven,pamoja na Mchezaji wa heshima.
Ndimbo
amesema zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo
ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao
hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.
"Kila
mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya
vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti
kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.
"Wachezaji
ambao walishinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu ni nimshambuliaji wa
Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze
(Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
"Wengine
ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa
Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John
Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari),
mshambuliaji wa Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa
Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili),"amesema Ndimbo.
Ambapo
wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na
fedha Sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.
No comments:
Post a Comment