Elimu : Taasisi ya ELIMU AFRIKA yaandika historia Chanya ya Elimu ya Tanzania na wadau mbalimbali. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Mar 2018

Elimu : Taasisi ya ELIMU AFRIKA yaandika historia Chanya ya Elimu ya Tanzania na wadau mbalimbali.



Taasisi binafsi inayojihusisha na maswala ya utoaji wa mafunzo ya elimu nchini Tanzania Elimu Afrika, tarehe 24.3.2018 imefanya kongamano lake la elimu katika ukumbi wa shule ya msingi Arusha ambapo wametoa mafunzo kwa jamii ikiwemo elimu ya bima, usalama barabarani, mafunzo ya habari na elimu ya umuhimu wa lugha ya alama.

Taasisi hiyo inayoongozwa na mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika, Mwl.  Danieli Urioh inayojishulisha mara zote  na utoaji wa elimu kwa umma kupitia mtandaoni, semina na matamasha mbali mbali.

Mkurugenzi wa Taasisi ya  Elimu Afrika Mwl. Daniel Urioh .
Katika kongamano mgeni rasmi alikuwa Prof. Raymond Mosha ambaye ni mkufunzi kutoka chuo cha Makumira na Nelson Mandela mkoani Arusha.


Kwa upande wake Mgeni rasmi amesema elimu inayowafaa wananchi ni elimu ambayo inamisingi na maadili na usawa ndani yake kwani itamjenga msomaji kimaadili na kiuadilifu.

Pia amewataka wasomi watumie elimu yao kuwasaidia watu wengine katika kuwapa elimu ili kuinua sekta hiyo ya elimu kwa maendeleo ya nchi.


Mwanafalsafa Prof. Raymond Mosha.

Wageni waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kutoka mkoani Arusha, Koplo Athilio Choga, wawakilishi wa NMB, Severina Gabrieli mwandishi wa vitabu, Janeth Akyoo mwalimu na mjasiriamali ,

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbali mbali wa Elimu, wakiwemo wanafunzi na viongozi wa taasisi mbali mbali za utoaji wa elimu.

Wageni waliohudhuria mkutano wa Elimu Afrika wakiwemo wanafunzi na wadau wa elimu nchini.


Kwa upande wa mtoa Mada kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha, Koplo Athilio Choga amewataka watumiaji wa barabara kuheshimu sheria zilizowekwa na mamlaka ya usalama barabarani ili kuepuska ajili za barabarani.


Hatahivyo amesema ajali nyingi zinazo tokea babararani husababishwa na ukaidi wawatu kuto kuheshimu sheria hizo ,jambo ambalo ni changamoto katika kuzuia ajali hizo.

Pia amesema kwa upande wa baadhi ya wanawake wamekuwa wakikaidi kuvaa kofia ngumu wakihofia kuharibu nywele, mawigi na mapambo mbalimbali.

Muelimishaji wa Sheria na Masuala yahusuyo Usalama Barabarani kutoka ofisi ya kikosi cha Usalama Barabarani  mkoani Arusha, Koplo Athilio Choga akitoa elimu ya usalama bara barani.


Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya utoaji wa habari na matangazo Kismaty Advert Media Madam Mary Mollel ameeleza faida ya uwepo wa vyombo vya habari nchini hususani uwepo wa mitandao ya kijamii unavyo saidia kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini. Ikiwemo kuhabarisha umma, kukosoa, kuelimisha, kukuza lugha na kuimarisha amani.



Mkurugengi wa Kismaty Advert Media Co. Ltd Madam Mary Mollel
Sambamba na hayo mfanyakazi wa kampuni hiyo Nickson Sawe ameelezea faida ya kuwa na elimu ya uandishi wa habari ili kumfanya mwandishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.

Na kueleza wapo baadhi ya watu ambao hawana elimu ya kutosha juu ya uandishi wa habariambao hushusha thamani na hadhi ya tasnia hiyo hapa nchini.

Mfanyakazi wa Kismaty Advert Media, Nickson Sawe


Katika kongamano hilo mwalimu wa lugha ya Alama kwa walemavu wasiosikia Bi Linda Malisa ameeleza faida ya lugha ya alama husaidia watu kuweza kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kusikia.


Nakuezeza faida ya lugha hii husaidia kuburudisha, kuokoa muda,kuleta usawa katika jamii kumuwezesha mlemavu kufanya kazi zake kwa ufasaha na kushiriki vyema katika shughuli za kulijenga taifa.


Hivyo ameitaka jamii na walezi kujifunza lugha ya alama na kuwapeleka shule watu wenye ulemavu wa kusikia na kuto waficha ili kujenga usawa wa haki kwa walemavu.


Pia ameeleza lugha hii hutumia viungo vya mwili wa binadamu kuanzia kitovuni kuelekea juu.



Mwalimu wa lugha ya Alama na Afisa Elimu wa Taasisi ya Elimu Afrika Bi. Linda Malisa


Naye dokta Nguma ambaye ni mdau wa elimu na mjasiriamali binafsi amesema utoaji wa elimu ni muhimu kwa kizazi kijacho kwani ndiyo urithi pekee unaodumu.


Pia amesema elimu ya Afrika haina hadhi ya kiafrika nahii ni kutokana na kurithi elimu kutoka kwa wazungu na watu husoma kwa kuwa wamepata fursa ya kusoma lakini wanachokisomea sio kipaji chao jambo ambalo wapo wasomi wengi katika Afrika lakini hakuna maendeleo.



Dokta.. Nguma mdau wa elimu na mjasiriamali

Elimu afrika imekuwa ikitoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, makongamano pamoja na mikutano mbalimbali ya elimu hapa nchini kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu na kujadiliana kubadilishana mawazo kwa lengo la kukuza elimu hapa nchini na hatimaye nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad