Utalii : Kamati ya Kudumu ya Bunge la Ardhi , Maliasili na Utalii Yatembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 2 September 2017

demo-image

Utalii : Kamati ya Kudumu ya Bunge la Ardhi , Maliasili na Utalii Yatembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga


DSC_1422
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, kutembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga leo. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atashasta Ndetiye (wa pili kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo, Nape Nnauye (kushoto) na Shaban Shekilindi (kulia).
DSC_1429
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia sehemu ya barabara iliyomeguka ndani ya eneo la Mapango ya Amboni.
DSC_1433Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakisikiliza maelezo kuhusu mapango hayo kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora.
DSC_1437Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea mapango ya Aboni Jijini Tanga leo.
DSC_1441Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kuingia ndani ya mapango ya Amboni. Mhandisi Makani alisema mipango ya Serikali ni kutambua vivutio vya aina mbalimbali ikiwemo vya mambo ya kale kama yalivyo mapango ya Amboni kuviboresha na kuvitangza ili vichangie zaidi katika pato ta taifa.
DSC_1450
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipata maelezo ya vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Mapango ya Amboni kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto).
DSC_1465Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni. Wajumbe hao waliishauri Serikali kuongeza thamani ya mapango hayo kwa kuboresha miundombinu na vivutio vilivyopo pamoja na kuvitangaza ili yachangie zaidi kwenye mapato ya Serikali.
DSC_1472
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kulia) na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia vivutio mbalimbali vya maumbo asilia ikiwemo ya wanyama na alama za kuabudia vilivyomo ndani ya mapango hayo.
DSC_1478
Muoneshaji wa Kujitolea katika Mapango ya Amboni, Othman Mangula (kulia) akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii moja umbo la asili lenye taswira ya Chui ndani ya Mapango ya Amboni ambapo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii ndani ya mapango hayo.
DSC_1443
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Dkt. Iddi Mfunda (kulia) na Muwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Canisius Karamaga (wa pili kulia) wakiangalia baadhi ya vivutio katika mapango ya Amboni.
DSC_1483
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakiwa ndani ya mapango ya Amboni.
DSC_1496
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akipenya kwenye njia nyembamba iliyopo ndani ya mapango ya Amboni.DSC_1506
Moja ya umbile la asili lililojitengeneza ndani ya mapango ya Amboni likiwa na taswira ya kwato za ngo'mbe.
DSC_1507
Maumbo mbalimbali ya asili yenye taswira ya viumbe ni moja ya kivutio kikubwa ndani ya mapango ya Amboni, Pichani ni umbo la asili lenye taswira ya matiti ambalo lipo ndani ya mapango hayo.
DSC_1524
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akimsaidia Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungu Ardhi, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya kushuka katika moja ya mteremko uliopo ndani ya mapango hayo.
DSC_1531
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Canisius Karamaga akifurahia jambo ndani maporomoko hayo.
DSC_1552
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Alan Kijazi akiwa ndani ya mapango hayo.
DSC_1568
Picha na; Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *