Michezo : Mbunge Mussa Aipiga Jeki Timu ya African Sports ya Tanga - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 27 September 2017

Michezo : Mbunge Mussa Aipiga Jeki Timu ya African Sports ya Tanga



Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African
Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga


Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akisalimiana na wachezaji wa timu ya Jang'ombe ya Zanzibar ambao wameweka kambi mkoani Tanga wakati alipokwenda kukabidhi vifaa kwa timu ya African Sports.





TIMU ya African Sports “Wanakimanumanu”imepata msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi daraja la pili itakayoanza kutimua vumbi.

Vifaa hivyo ambavyo ni seti ya viatu vilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge Mussa alisema ameamua kutoa vifaa hivyo ili kuweza kuihamasisha kufanya vizuri katika mashindano hayo na hatimaye kuweza kurudi ilipotoka.

Alisema licha ya timu hiyo kushuka daraja hivi sasa wanapaswa
kujiimarisha na kucheza kwa umakini mkubwa ili kuweza kucheza michuano ya ngazi za juu.

“Mimi ni Mbunge lakini pia ni mwana michezo hivyo nitahakikisha nazisapoti timu za mkoa huu kwa lengo la kurejea kwenye makali yao ya zamani kwani michezo ni ajira “Alisema.

Nay kwa upande wake,Mweka Hazina wa timu hiyo,Sad Juma alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia timu hiyo kuondokana na uhaba uliokuwepo.

“Kama unavyojua sisi tulikuwa na uhaba wa vifaa vya michezo hususani viatu na nyenginevyo hivyo alichotupa mbunge tunamshukuru lakini tutakuwa nawe bega kwa bega “Alisema.

Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na mashindano hayo wakiwa na kikosi imara ambacho kimedhamiria kupata mafanikio.




Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments:

Post a Comment