Utalii : Wananchi waomba fidia ya Mazao yanayoharibiwa na Wanyamapori - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Aug 2017

Utalii : Wananchi waomba fidia ya Mazao yanayoharibiwa na Wanyamapori










Na Ferdinand Shayo,Arusha.



Wananchi wa Vijiji na Kata zinazopakana na hifadhi ya taifa ya Arusha (ANAPA) wameiomba serikali kupitia kitengo cha Maliasili kuwalipa inayotokana na uharibifu wa mazao ya chakula unaofanywa na wanyamapori.



Wakiwasilisha malalamiko kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Meru , Diwani wa kata ya Nkoanekoli Wilson Nanyaro alisema kuwa jumla ya ekari 6 za mazao zimeharibiwa na wanyamapori hivyo wameiomba idara ya Maliasili ili kunusuru kaya 12 na uhaba wa chakula.



Nanyaro alisema kuwa katika kipindi hiki cha mavuno wananchi hao wamepata mazao machache sana kutokana na mazao yao kuliwa na nyani ambao hutoka hifadhi hiyo ya taifa.



Diwani viti Maalumu kata ya Embaseny Agness Lambo Alisema kuwa wamekua wakitoa taarifa kwa idara hiyo ila wakichelewa kuzifanyia kazi kwa muda muafaka hivyo kusababisha maumivu ya kiuchumi kwa wananchi ambao hutegemea kilimo kujikwamua kimaisha.



“Wananchi waliokubwa na adha hii wanaishi umbali mrefu kutoka katika hifadhi ya Arusha tumekua tukitoa taarifa ila Maafisa wa Maliasili wamekua wakichelewa mara kwa mara hivyo kusababisha wananchi kutokupata haki stahiki” Alisema Lambo



Afisa Maliasili Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bernad Saruni amekiri kuwepo kwa tattizo hilo na tayari wameanza kuwalipa fidia wananchi wa kijiji cha Leguruki,Ngarinanyuki fedha ambazo ni kifuta machozi baada ya uharibifu huo kutokea.

Hata hivyo amewataka Wananchi kuzingatia vigezo muhimu ili kufidiwa ikiwemo kufanya shughuli zao umbali wa mita 500 kutoka katika mpaka wa hifadhi ya taifa ya Arusha na pia kutumia njia za asili kuyalinda mazao yao yasiharibiwe na wanyama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad