Utalii : TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Aug 2017

Utalii : TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China


BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeridhishwa na idadi kubwa ya watii kutoka nchini China na kuelezea kuwa endapo kutakuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kutasaidia kupunguza gharama za safari na pia kuchochea utalii.


Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa juzi kuwa endapo kutakuwepo na ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka China, idadi kubwa ya watilii kutoka nchi hiyo itaongezeka na pia mataifa mengine, hivyo sekta ya utalii uchangia zaidi mapato ya serikali.


akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembeza waandishi waandamizi wa habari kutoka nchini China katika hifadhi za Ngorongoro Crater na Manyara,Jaji Mihayo alisema vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ni tunu kubwa kwa taifa na pia vinawaleta watalii kutoka sehemu mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi(wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja waandishi Waandamizi wa habari kutoka China walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara na kujionea fahari ya Tanzania. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.


“Ujio wa wanahabari hawa ni fursa kwetu kwani watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa machapisho na habari nchini kwao juu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania,” alisema na kutoa wito kwa waandishi wa ndani kuunga mkono jitihada hizo.


Alisema waandishi hao kutoka China wameonyesha nia ya dhati ya kuvitangaza vivutio vyetu na hivyo kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania, zoezi hilo litakuwa la mafanikio makubwa.


Aliongezea kuwa China ni nchini yenye watu wengi Dunia hivyo kupitia waandishi hawa watakwenda kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo kupitia makala na machapisho mbalimbali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akizungumza na waandishi waandamizi wa habari kutoka China mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.


“changamoto kubwa waliyoiona ni gharama ya usafari wa ndege ni kubwa kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja,” alisema Jaji Mihayo na kuongezea kuwa usafiri wa anga utakapo imarishwa utachochea idadi kubwa ya watalii kutoka China. Alisema tayari Rais Magufuli alishaahidi kuleta ndege Kubwa itakayofanya safari ndefu hivyo itasaidia kupata soko la watalii kutoka china kuongezeka na itasaidia kuongeza mapato katika sekta ya utalii.


Alisema pia Halmashauri na wawekezaji katika hoteli mbalimbali zilizopo katika maeneno ya vivutio vya utalii waunganishe nguvu ili kutatua changamoto za barabara kwani imekuwa ni kero kwa wageni. Miundombinu ya barabara kuelekezea maeneo ya hotel pia katika vivutio ni mbovu hivyo Serikali kushirikiana na sekta binafsi wajipange kuboresha miundombinu ili iwe rafiki na kuvutia watalii zaidi alisema Jaji Mihayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akimkabidhi zawadi kwa Mhariri Msaidizi kutoka China Daily Media Group, Bw. Kang Bing(kulia) mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania. ziara hiyo iliwajumuisha wahariri sita kutoka vyombo mbalimbali vya nchini China.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Bibi Devota Mdachi alisema ujio wa wanahabari hawa ni mwendelezo wa juhudi za TTB katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kufanya idadi ya watalii kuongezeka. “ tumepokea jumla ya waandishi sita kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Nchini China ikiwa ni njia mojawapo ya kuendeleza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii katika nchi hiyo,” alisema Bi.Mdachi Alisema tumejipanga kukuza soko la utalii kwa kuongeza idadi ya watilii kutoka china kwani ni moja ya nchi yenye watu wengi duniani hivyo kwa njia ya kuwatumia waandishi wa habari itasaidia kuvitangaza vivutio vyetu kwa urahisi zaidi.


Aliongezea kuwa pamoja na kuvitangaza vivutio vyetu ni lazima kuboresha miundombinu hususani barabara katika maeneno ya vivutio ili kuwapa urahisi watalii kufika katika maeneo ya hifadhi. “Wamevutiwa sana na vivutio vyetu na wameahidi kuwa mabalozi wetu nchini kwao wa kuvitangaza vivutio vyetu,”alisema Bi Mdachi Alisema matumaini yetu kupitia ujio huu ni kupata watalii wengi kutoka nchini China na njia hii ya kutumia waandishi wa habari tutaendelea kuitumia kwa nchi nyingine ili nao wawemabalozi katika nchi zao na hatimae kukuza sekta ya utalii nchini.


Akiongea kwa niaba ya watalii wengine Mhariri Msaidizi kutoka China Daily Media Group Bw. Kang Bing alisema wamefurahi kuona vivutio vilivyopo Tanzania pamoja na ukarimu wa watanzania. “Tulitembelea maeneo mbalimbali kama Ngorongoro na ziwa Manyara na kuona wanyama na ndege mandhari nzuri na hili limekuwa somo jipya kwetu,” alisema Bw. Bing Alisema tutakwenda kuwa mabalozi wa kutangaza maeneo ya vivutio vya utalii kupitia machapisho na makala mbalimbali ili kuchochea idadi ya watalii kutoka china kuongezeka.


Changamoto kubwa ni kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo ya hifadhi na pia kuwekeza kwenye usafiri wa anga kwa kuwa na safari za moja kwa moja. Jumla ya waandishi sita kutoka Beijing Press Group, China Daily, International Liaison Drpartment, English news service na China Radio International walitembelea hifadhi ya Ziwa Manyara na Ngorongoro Crater.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad