Teknolojia : Bill Gates ajiunga Instagram akiwa Tanzania, arusha picha za Muheza Tanga - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 12 August 2017

Teknolojia : Bill Gates ajiunga Instagram akiwa Tanzania, arusha picha za Muheza Tanga




Jarida la Fobers limeripoti kuwa tajiri namba moja duniani Bill Gates amejiunga Instagram akiwa nchini Tanzania na kurusha picha tatu ikiwemo aliyopiga na watoto akiwa Muheza mkoani Tanga.

Gates ameijunga na mtandao huo wa kijamiii kwa jina la thisisbillgates na kurusha picha zake za kwanza tatu zote akiwa Tanzania.

Gates katika mtandao huo aliandika hiki, “Hello kutoka Tanzania, Instagram! Nimepata chakula cha mchana kizuri nikiwa na watoto wanaovutia katika Shule ya Msingi Kicheba Muheza na nikakutana na Upendo Mwingira ambaye amejikita katika kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele. Melinda na mimi tumekuwa tukija Tanzania kwa miaka mingi sasa. Huwa napenda kuona maendeleo nchi iliyoyafanya katika kuboresha afya na kutoa nafasi.”

Kwa Kiingereza aliandika hivi “Hello from Tanzania, Instagram! I just had a great lunch with some amazing kids at Kicheba Primary School in Muheza and met Upendo Mwingira, a remarkable physician who has dedicated her career to fighting neglected tropical diseases. Melinda and I have been coming to Tanzania for many years now. I always love seeing how much progress the country has made to improve health and provide opportunity. Plus, the scenery is stunning. Whenever I travel to places like this, I wish others could come along and meet the people I get to meet. I have no doubt it would leave them as optimistic as I am about progress happening around the world. I’ll be sharing photos from my adventures here on Instagram, and I hope you’ll follow along.”

No comments:

Post a Comment