RSA DAY 2017 : Taswira Mbalimbali ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani, Mkoani Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Jul 2017

RSA DAY 2017 : Taswira Mbalimbali ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani, Mkoani Dodoma



Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Taifa(Mwenye T-Shirt ya Blue) akiwa ameambatana na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Mohammed Mpinga ambae pia ni katibu wa Kamati ya usalama barabarani na Mlezi wa RSA Tanzania wakiwa wanaingia uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma baada ya kupokea maandamano ya Mabalozai wa usalama Barabarani yaliyofanyika mapema leo Mjini Dodoma (Makao makuu ya Nchi). Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus

Mgeni rasmi Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni pamoja na Kamanda wa Usalama barabarani Mohamed Mpinga pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa katika siku ya mabalozi wa usalama barabarani yaliyofanyika katika kiwanja cha mashujaa leo mjini Dodoma .

Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni akiwaanazungumza na mabalozi wa usalama barabarani pamoja na wadau mbalimbali ,wageni waalikwa leo mjini Dodoma.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Mohammed Mpinga akizungumza katika siku ya mabalozi wa usalama barabarani Mjini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha Elimu nchini Tanzania ASP Mosi Boniface Ndozeikaro akizungumza katika siku ya mabalozi wa usalama barani Dodoma .

Na.Vero Ignatus /Murtadhwa Elbahsan


Siku ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA) imefanyika Kitaifa mkoani Dodoma ambapo Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni amekuwa mgeni rasmi, shughuli hiyo imefanyika katika viwanja vya mashujaa na imewashirikisha mabalozi mbalimbali Tanzania bara na Visiwani.

Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama Taifa John Seka amesea kuwa lengo kuu la siku hiyo ni kuweza kuleta uhamasishaji kwa wananchi ili waweze kupata elimu ya usalama barabarani na wasione ni jukumu la jeshi la polisi peke yake, kukuza mahusiano na jeshi la polisi pamoja na mabalozi kufahamiana zaidi na kuwapongeza mabalozi kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya ya kujitolea.


Kwa upande wake kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani ambae pia ni katibu wa Baraza la usalama barabarani Taifa DCP Mohammed Mpinga amesema kuwa takwimuza vifo na majeruhi zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea zinaathirika sana na tatizo hili hivyo bado tunalo jukumu kubwa la kupingana na ajali za barabarani


Ameainisha takwimu za ajali kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017 zimepungua kwa asilimia 44 vifo vimepungua 13% majeruhi 30% ambapo wa asilimia kubwa RSA inahusika kwa kiwango kikubwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi changamoto kutambua juhudi za usalama barabarani wanaojitole.


Mpinga ambae pia ni mlezi wa( RSA)amewapongeza mabalozi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kukabiliana na ajali za barabarani kwa kuonya kukaripia pale wanapoana mwenendo mbaya wa madereva pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani


“ Muendelee kujitoa kama vile ambavyo mnavyojitoa kwani mnalirahisishia kazi jeshi ,mmekuwa mkiokoa maisha ya watu wasife kwa uzembe kwaajali za kujitakia “alisema .






Amezitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na vifaa vya lkutendea kazi,ubovu wa barabara na miundombinu,ukosefu wa alama za barabarani,utashi wa kisiasa ,wadau wanaona suala la usalama barabarani siyo la kwao na haliwahusu.






Mkuu wa kitengo cha Elimu nchini Tanzania ASP Mosi Boniface Ndozero amesema kuwa mambo mawili lazima yazingatiwe, “ni vyema kuzingatia na kufuata alama za usalama barabarani yote yakizingatiwa ajali zitapungua kabisa” amesema kuwa jeshi lapolisi nchini kitengo cha elimu limejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa elimu wanayoitoa inawafikia walengwa pamoja na hayo amesema jeshi la polisi limejipanga kutoa elimu kwa wanafunzi mashuleni kuhusu elimu ya usalama barabarani






Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa wanamipango endelevu katika mji wa Dodoma ili ujio wa serikali usije ukaongeza vifo na ajali kwani wamejipanga kuthibiti ajali za barabarani






Ikumbukwe kuwa RSA imesajiliwa rasmi mwaka 2014 kama taasisi isiyo ya kiserikali ikiwa na wanacham 10 hadi sasa wapo zaidi ya 60,000 kwenye majukwaa ya mitandao wa kijamii (Whatsap, Facebook, Twitter, Instagram nk.), wapo wakurugenzi 8, kanda 5ambazo ni kanda ya kusini, kanda ya kati, kanda ya kaskazini ,kanda ya mashariki,kanda ya ziwa na kanda ya nyanda za juu kusini, wapo maadimini 20 kwenye majukwaa hayo ya mitandao ya kijamii.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Skauti wa mjini Dodoma .


Mabalozi wa usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja .

Afande Jahnson Kahatano mkurugenzi wa barabara Sumatra Taifa akizungumza kaika siku ya mabalozi wa usalama barabarani.


RPC wa mkoa wa Dodoma Afande Mambosasa akizungumza.


RTO wa mkoa wa Dodoma Marson Mwakyoma akizungumza.

Balozi Augustus Fungo akizungumza katika siku ya Mabalozi wa usalama barabarani leo Dodoma .


Mratibu wa RSA wa kanda ya kati Kelvin John akizungumza.

Mabalozi wa Usalama barabarani waliovalia tshrit za blue na nyekundu wakiwa katika picha ya pamoja katika siku yao iliyofanyika  Dodoma .

Waendesha pikipiki wakiwa katikaa maandaano katika siku ya (RSA DAY)yaliyofanyika mjini Dodoma .
Waendesha bajaji wakiwa maandamano hayo .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad