Matukio : RC Kilimanjaro yupo ziarani Wilayani Rombo - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Jul 2017

Matukio : RC Kilimanjaro yupo ziarani Wilayani Rombo


Na Mwandishi wetu, Rombo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira Jumatano amefanya ziara ya kikazi wilayani Rombo , ambapo alianza kwa kukutana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hiyo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kabla ya kufika kituo cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania upande wa Holili.


Aliendelea na ziara ndani ya wilaya kupitia eneo la mpaka wa Kenya na Tanzania linalotajwa kama njia ya panya ya kutorosha magendo na mahindi toka Tanzania kwenda Kenya.


Ziara yake ilifikia kituo kingine cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania cha Tarakea na kisha kumalizia ziara yake eneo la msitu wa miti ya kupandwa wa Rongai eneo la Kamwanga. Ziara ilianza saa tatu asubuhi na kumalizika sa kumi na mbili jioni.


Mhe Mkuu wa Mkoa alisisitiza kila Mtumishi kutimiza wajibu wake kwa kuwa na UTU NA UZALENDO.

"...Lazima tumpime mtumishi kwa kila siku amefanya kazi gani katika ofisi yake - tangu mlinzi, mfagizi hadi afisa wa juu. Ni lazima tuwajibike. Watumishi lazima mtambue nafasi zenu, mziheshimu na kujua kuwa kazi na nafasi yako ni kiungo cha nafasi na kazi ya mwenzako..."alisema Mhe. Mghwira.
Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe Agnes Hokororo (kulia) alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani humo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akilakiwa na watumishi akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akitambulishwa kwa watumishi na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe Agnes Hokororo alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani humo


Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akisaini vitabu vya wageni alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akisaini vitabu vya wageni alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na watumishi alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na watumishi alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiwa na uongozi wa wilaya tayari kuanza ziara yake ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akioneshwa maeneo na Katibu Tawala Bw. Abubakar Asenga wakati wa ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akitembezwa maeneo mbalimbali katika ziara ya kikazi wilayani Rombo

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na wafanyabishara na wananchi katika ziara ya kikazi wilayani Rombo.

Post Top Ad