Habari : Mtangazaji Mkongwe wa Redio Aliyeanzisha Neno 'Bongo Flava' Mike Mhagama Aanzisha Kipindi cha Historia ya Muziki Huo - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday, 27 July 2017

Habari : Mtangazaji Mkongwe wa Redio Aliyeanzisha Neno 'Bongo Flava' Mike Mhagama Aanzisha Kipindi cha Historia ya Muziki Huo








Mike Mhagama - Mtangazaji Mkongwe.




Mtangazaji mkongwe wa redio na miongoni mwa watangazaji wa kwanza kabisa wa redio za FM nchini Tanzania, Mike Mhagama, amekuja na kipindi (podcast) kiitwacho Maktaba ya Bongo Flava, ambacho atakitumia kuelezea historia ya muziki huo. “Maktaba ya Bongo ni makala itakayojikita zaidi katika kuzungumzia muziki wa kizazi kipya, kuanzia historia yake yaani ilikotoka,ilipo na inakokwenda,” anasema.




“Pamoja na majadiliano ya nini kifanyike zaidi kupanua wigo wake wa washabiki na biashara duniani.Msukumo wa kuandaa kipindi hiki ulitokana na maombi ya mashabiki wenyewe kuomba kuwepo na makala maalum kama haya hasa kwa vijana ambao hawafahamu historia halisi,” ameongeza.




“Pili, kuweka facts sawa kwani kumekuwa na upotoshwaji mkubwa sana na wa makusudi katika historia ya muziki huu.Mwisho ni ushawishi wa rafiki yangu Fredrick Bundala ambaye alinisihi kushare ninachokifahamu kuhusu muziki huu ili wengi wa pate kunufaika na kumbukumbu za muziki wa kizazi kipya. Natumaini wengi watafurahi na kuelimisha pia.”




Kipindi hicho kitakuwa kikitoka kila wiki siku ya Alhamis kupitia jukwaa la kwanza Afrika la podcast, Afripods. Unaweza kusikiliza kipindi hicho kwa kuclick hapa > http://bit.ly/2h4ta2K. Unaweza kusikiliza kipindi hicho kwa kudownload app ya Afripods kwenye App store na Google Playstore.




KUHUSU MIKE MHAGAMA




Mike Mhagama ni moja ya watangazaji na Madj wa kwanza kabisa wa redio za FM nchini Tanzania. Anajulikana kama mmoja wa watu wenye ushawishi zaidi katika miaka ya 90 enzi muziki wa kizazi kipya unachipukia nchini. Akiwa Radio One Stereo, Mike alikuwa mtangazaji wa vipindi vitatu vya kila wiki vilivyofanikiwa sana. Kipindi kilichokuwa maarufu zaidi kilijulikana kama DJ Show ambapo aliamua kuwapa muda wa hewani wasanii wachanga wa nyumbani.




Katika kipindi hicho, Mike hakucheza tu muziki wao, lakini aliwaalika na kufanya nao mahojiano, kitu ambacho enzi hizo hakikuwa kikifanyika sana. Aliwapa wasanii chipukizi jukwaa la kueleza mitazamo yao kupitia muziki. Mike ndiye muasisi wa neno "Bongo Flava", lililoundwa mwaka 1996 kuupa muziki wa enzi hizo utambulisho wake.







Jina hilo lilishika na kilichobaki ni historia tu. Kwa sasa Mike anaishi Los Angeles,California nchini Marekani akifanya kazi za benki. anaand works as a Banker. Ni msomi wa shahada ya masuala ya Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment