Matukio : Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan Awaongoza maelfu kuiaga miili ya Wanafunzi 32, Walimu 2 na Dereva 1 waliofariki kwa ajali Wilayani Karatu,Mkoani Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 8 May 2017

Matukio : Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan Awaongoza maelfu kuiaga miili ya Wanafunzi 32, Walimu 2 na Dereva 1 waliofariki kwa ajali Wilayani Karatu,Mkoani Arusha

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM , Komredi Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Waziri wa Elimu wa Tanzania , Prof. Joyce Ndalichako akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Waziri wa Elimu wa Kenya, Mhe. Fred Matiang'i akiwahutubia na kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Mwakilishi kutoka Zanzibar , akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.


KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.


Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Askofu Josephat Lebulu akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Arusha waliokuja kuiaga miili ya wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Prof. Joyce Ndalichako akiongozana na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu akielekea kutoa heshima za mwisho kwa wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Mbunge wa Arusha Mhe. Godbless Lema na Mkewe wakiongozana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kwenda kutoa heshima zao za mwisho wanafunzi 32 ,walimu 2 na Dereva 1 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki kwa ajali ya gari tarehe 06:05:2017 wilayani Karatu Mkoani Arusha. Picha Zote na Gadiola Emanuel.
  
Na Vero Ignatus, Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi wa Arusha kuiaga miili ya wanafunzi 32 , Walimu 2 na Dareva 1 wa shule ya Lucky Vincent ya Arusha ambao waliofariki katika ajali ya gari tarehe 6 mei 2017 saa tatu asubuhi katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Katika shughuli hiyo ya kuiaga miili hiyo ambayo imehudhuriwa viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi amesema kuwa ipo sababu ya jeshi la polisi wazazi pamoja na waalimu kuzingatia usalama barabarani.

Hata hivyo amemshukuru Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kuguswa na msiba huu ambapo amemtuma waziri wa elimu kutoka nchini Fred Matiang'i kuja kushiriki katika msiba huo mzito wa Kitaifa.

Amesema kuwa msiba huu siyo wa taifa la Tanzania peke yake bali ni msiba wa Afrika kwa ujumla ambapo amesema pigo hili linatufanya kufanya marekebisho ya matendo yetu.

Ametoa wito kwa madereva kuwa makini na kuwa waadilifu wawapo barabarani kubeba abiria kulingana na uwezo wa gari,wametakiwa kukumbuka kuwa serikali inapiga vita vilevi , madawa ya kulevya pamoja na mwendo kasi.

Amelitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wafuatilie na kuhakikishekuwa alama za barabarani zipo sawa ,pia kuweka vibao mahali panapotakiwa kwani
Msiba huu umetupa majonzi mengi watanzani na kila mtu. Aidha amewataka wamiliki wa shule pamoja na waalimu kuhakikisha kuwa magari ya shule yanachukua abiria kwa uwezo unaotakiwa kwani haipendezi kila mara kusikia taifa linakubwa na misiba
Ikumbukwe kuwa ajali hii iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 walimu 2 na dereva 1 ilisababishwa na gari aina ya T 871 BYS coaster rosa kuacha njia na kudumbikia korongoni, ambapo mashuhuda wa ajali wanadai "ni Mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na dereva kutokuwa mzoefu na njia hiyo",ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumamosi 6 Mei 2017 majira ya saa tatu asubuhi katika mteremko wa mlima Marera kata ya Rhotia, wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment