Matukio/ Afya : Majeruhi wa Ajali ya Karatu wasafirishwa kwenda Marekani kwa matibabu zaidi - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


14 May 2017

Matukio/ Afya : Majeruhi wa Ajali ya Karatu wasafirishwa kwenda Marekani kwa matibabu zaidiMbunge Mhe. Lazaro Nyalandu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakiwaaga Wanafunzi watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vincent Arusha, waliojeruhiwa kwenye Ajali iliyotokea Rhotia ,Karatu Arusha, Wakisafirishwa kwenda Marekani kwa matibabu zaidi.

Majeruhi hao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Mt. Meru Jijini Arusha, ambapo wenzao 32, walimu 2 na dereva 1 walifariki kwenye ajali hiyo mnamo tarehe 06:05:2017 katika kijiji Marera, Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Kifaa maalum kikiwapandisha watoto hao kuingia kwenye ndege maalum kuelekea Marekani kwa Matibabu

Muonekano wa ndani ya ndege.

Post Top Ad