Maisha : Mfuko wa Jamii, PPF yatoa msaada wa vifaa Tiba , Morogoro - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 20 May 2017

Maisha : Mfuko wa Jamii, PPF yatoa msaada wa vifaa Tiba , Morogoro




Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian.



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.



Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF. Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga akitoa ufafanuzi mchache jinsi alivyokuwa anaufahamu Mfuko wa Pensheni PPF. Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakielekea wodini.





Wagonjwa wakitumia mashuka na vitanda vilivyotolewa na PPF. --- Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini. Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini. Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha. Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment