Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milioni nne kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha juzi Bi.Faith Mushiro kwaajili ya kukarabati madarasa manne ambayo hujaa maji kipindi cha mvua hali ambayoilikuwa ikiwasababishia wanafunzi kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku.
Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko pamoja na timu yake wakikagua madarasa yanayojaa maji kipindi cha mvua.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa benki ya CBA mara baada ya kupata msaada wa shilingi Millioni nne kwaajili ya ukarabati wa madarasa
Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko pamoja na timu yake wakikagua madarasa yanayojaa maji kipindi cha mvua.
Na Pamela Mollel,Arusha
Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha iliyokuwa ikikabiliwa na changamoto ya madarasa kujaa maji imepatiwa msaada wa kiasi cha shilingi Milioni nne na benki ya biashara ya Africa (CBA) kwaajili ya ukarabati wa baadhi ya madarasa
Akikabidhi hundi katika shule hiyo juzi Mkurugenzi wa CBA Gifti Shoko alisema kuwa lengo la msaadahuo ni kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya kutoa maji katika madara pindi mvua zinaponyesha hali inayosababisha kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku
Alisema kuwa msaada huo utumike kama ulivyo kusudiwa kuboresha madarasa hayo kwani ubora wa elimu unaletwa na mazingira mazuri ya watoto kusomea
‘’Hapa nawaona Marais, mawaziri wa kesho pamoja na wafanyakazi wazuri wa bank yetu hivyo hatuna budi kutuoa msaada huu ikiwa kama mchango wetu wa kuboresha sekta ya elimu na tunawahidi hatutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia kadri ya uwezo wetu ‘’
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Faith Mushiro akitoa neon la shukrani alisema kuwa wanafunzi wa darasa la tano na la sita ndiyo hasa walikuwa wakipata hadha hiyo ya kuondoa maji madarasani pindi mvua zinapoanza kunyesha
Aidha alisema kuwa zaidi ya vipindi viwili hadi vitatu vya asubuhi hushindwa kuhudhulia kutokana na changamoto hiyo hivyo kupitia msaada huo wanafunzi watasoma katika vyumba vya madarasa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma
Awali akisoma Risala mwalimu wa shule hiyo Bw.Simon Mbawala kwa niaba ya shule hiyo alisema kuwa pamoja na msaada waliopatiwa bado shule inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa makataba ya kuhifadhi vitabu ,kuharibika kwa sakafu za madarasa pamoja na kupasuka kwa vioo vya madirisha
Hata hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mssada huu wa ujenzi wa vyumba vinne ambayo vilikuwa na tatizo la kuvuja kwa maji kutokana na bati zake kuwa chakavu hali iliyokuwa ikiwathiri sana wanafunzi na walimu hasa ikifika wakati wa kufundisha.
No comments:
Post a Comment