Maisha : Dk. Mengi Akarimu Wafaransa - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Apr 2017

Maisha : Dk. Mengi Akarimu Wafaransa


MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini. Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro.


Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza. Alisema jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla.Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)


“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili. Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia. Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi. Aliwatakia wageni wake chakula chema..Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es Salaam.


Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano. “ …Business and friendship goes Together..” alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa kubahatisha unakua. Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye 'cocktail' kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Eng. Raymond Mbilinyi (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika halfa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi 'Application' ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville.'Meet and Greet' ikiendelea kwa wenyeji na wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mwimbaji mkongwe nchini Mzee Zahir Ally Zoro akitumbuiza kwenye hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Meza kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akisherehesha wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk Mengi kwenye hoteli Serena jijini Dar es SalaamMwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha juu na chini ni wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini Ufaransa wakijumuika na wenyeji wao katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde alikuwa miongoni mwa wageni waaalikwa katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad