Teknolojia : Telkom and Business Connexion yazindua BCX, Suluhisho la Teknolojia mahiri inyoongoza barani Afrika - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 11 March 2017

Teknolojia : Telkom and Business Connexion yazindua BCX, Suluhisho la Teknolojia mahiri inyoongoza barani Afrika





Mashirika na asasi zote ambazo hazikumbatii na kukubali mfumo wa kuendesha biashara kidigitali zinajiweka pabaya kutemwa na wateja wao.


Kutokana na tishio hili, Telkom and Business Connexion inazindua rasmi BCX, mfumo mpya na wa kisasa kidigitali unaoongoza barani Afrika, unaotumika kurahisisha mawasiliano ya miamala ya biashara na mawasiliano.


Toleo hili jipya la teknolojia, lililoandaliwa kwa ushirika kati ya Telkom Business na Business Connexion, ni la kipekee katika ufumbuzi wa kitekinolojia unaosambaa kwa kasi barani Afrika kuwezesha na kurahisisha mawasiliano na ufanisi wa kibiashara.


“Uzinduzi wa BCX kwa kweli unafungua ukurasa mpya katika mwelekeo wa ufanisi wa kibiashara kwa tekinoljia pevu barani Afrika,” alisema Seronga Wangwe ambaye ni Mkurugenzi wa BCX Tanzania, katika hotuba yake ya ufunguzi aliyoitoa hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar Es Salaam.


“BCX imejengwa kutoka katika msingi imara wa Telkom Business yenye maarifa na elimu pevu ya miundombinu ya mawasiliano pamoja na taaluma ya muunganisho wa kibiashara inayojali kutoa huduma kwa ukaribu na unyenyekevu kwa wateja wake.


“BCX sasa ni bidhaa mpya ya mawasiliano barani Afrika yenye ufanisi wa kutoa huduma kwa umakini mkubwa’, aliongeza Bwana Wangwe.


Mfumo wa kidigitali uliopevuka unapewa kipaumbele na aina zote za biashara barani Afrika. Kwa sasa inaelewaka bayana kuwa kampuni yeyote ambayo inakwepa au kudharau kuendesha miamala yake kidigitali ipo hatarini kutorokwa na wateja katika mwelekeo wa kudorora kabisa!


BCX inatoa mwelekeo mpya popote barani Afrika katika kutoa huduma kidigitali ili kutoa huduma bora kibiashara kwa sasa na kwa muda mrefu kwa wateja wake.


“Hakuna kitu kilichonifurahisha zaidi leo hii kama uzinduzi huu mpya wa BCX,” alisema, mkuu wa BCX international ALTHON BEUKES.


BCX inaweka bayana aina ya mawasiliano na mahitaji yote ya makampuni yaliyomo barani Afrika katika kutoa ufumbuzi sahihi wa matatizo ya mawasiliano kibiashara, katika masoko yake ya ndani na hatimaye kupenya nje ya mipaka na kusambaa barani kote. Itasawazisha uwezo wa makampuni katika kujitanua kitekinolojia na mahitaji ya mawasiliano ya makampuni barani Afrika.


“BCX’s imetandaza nyayo zake kibiashara barani Afrika ikiwa na makampuni tanzu katika nchi kama vile Kenya, Nigeria, Tanzania, Namibia, Zambia na Botswana, halikadhalika uwepo wake huko Dubai na Uingereza, inatufanya tuwe mfano pekee na bora kwa mwasiliano na washirika na wateja wetu wote wanaofanya biashara nasi barani Afrika na wale walio katika matarajio ya kujiunga nasi katika mwelekeo wa ufanisi kibiashara ili kuliongoza bara la Afrika kwenye ushindi wa nafasi za kibiashara,” aliongeza.


Uzinduzi wa BCX ni hatua ya mwisho katika kunyumbulisha Telkom Business na Business Connexion. BCX itaendelea kujikita ndani ya Telkom Group, lakini itajali kufanya biashara katika ufanisi mkubwa. Wafanyakazi wote wanafahamu umuhimu wa tekinolojia hii mpya na ofisi zote zina thamini bidhaa hii mpya ya mawasiliano. Kwa kuongozea, miamala yote ya kibiashara na wateja itajikita katika sura mpya ya utambulisho wa BCX.


BCX kwa kwenda mbele itaendelea kuangalia kwa umakini mahitaji ya wateja wake na kutoa ufumbuzi wa uhakika hususan kwa matumizi ya kompyuta, mawasiliano na ushirikainao wa karibu, na mnyumbulisdho wa kibiashara wenye usalama wa uhakika kwa mtandao pamoja na uchambuzi makini wa takwimu za kibiashara.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya BCX Tanzania Bw. Seronga Wangwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam katika uzinduzi wa kampuni ya BCX ambayo imejumuisha kampuni za Business connexion na Telkom katika hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Kulia ni meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw. Ebenezer Massawe.



Kutoka kushoto ni Bwa. Seronga Wangwe, (mwakilishi) kutoka Mozambique High Commission, Bwa.Frans Van Aardt- Councelor kutoka ubalozi wa Afrika kusin,Bi.Monica Patricio Clemente- Balozi wa Msumbiji, pamoja na Bwa.Althon Beukes- mkuu wa BCX International wakiwa katika picha ya pamoja.

. Mgeni rasmi Bw. Frans Van Aardt ambaye ni Councelor wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania. Akizungumza katika Uzinduzi wa kampuni ya BCX uliofanyika Hyatt hotel Dar es salaam
Mkuu wa BCX International Bw. Althon Beukes akizungumza na wageni katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni ya BCX, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
Wasanii kutoka kikundi cha Kigamboni Community Centre (KCC) wakitoa burudani ya ngoma za asili kwa wageni na waalikwa katika siku ya uzinduzi wa kampuni ya BCX nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Hyatt regency (the Kilimanjaro).
Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa BCX Tanzania
Bw. Seronga Wangwe (Mkurugenzi mtendaji wa BCX Tanzania) akizungumza na wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni hiyo siku ya jumatano katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam

No comments:

Post a Comment