Matukio : Bi. Dossi afungua kongamano la Wanawake, Tanga. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Mar 2017

Matukio : Bi. Dossi afungua kongamano la Wanawake, Tanga.



Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akifungua kongamano la Wanawake Jijini Tanga ambalo lilikuwa na lengo kuu la kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa wanawake ikiwemo fursa za kiuchumi sambamba na kupambana na dawa za kulevya kwa jamii lililofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga leo

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi wa pili kutoka kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa wakati wa kongamano la wanawake Jijini Tanga kuelekea siku ya wanawake dunia kushoto ni Rehema na Yahaya Seumbe ambaye ni Afisa kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii kwenye Jiji la Tanga wakifuatilia kongamano hilo.

Baadhi ya Wakina wanawake jijini Tanga wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo

Sehemu ya Umati wa wanawake wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo la wanawake wa Jiji la Tanga kuelekea siku ya wanawake Dunia ambapo kilele chake itakuwa ni Machi 8 mwaka huu

Baadhi ya waandishi wa habari jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo wa kwanza kulia ni Burhan Yakub wa gazeti la Mwananchi,Bertha Mwambele wa TBC TV na Sussan Uhinga wa Clous TV



Sehemu ya wakina wanawake Jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano la wanawake kuelekea siku ya wanawake ambapo kilele chake ni Machi 8 mwaka huu

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia Machi 8 mwaka huu mara baada ya kufungua kongamano la wanawake Jijini Tanga.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga baada ya kumalizika kwa kongamano hilo ambapo alisema kuelekea siku ya wanawake kutafanyika shughuli mbalimbali za kijamii
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad