Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema inahitaji kufanya utafiti wa kina kabla ya kutoa maamuzi dhidi ya kesi mpya inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Mariam Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus Muyela (40).
Hakimu Mkazi Thomas Simba amesema hayo Leo asubuhi wakati kesi hiyo ya mauaji ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa amuzi wa ifutwe au la kutokana na mabishano ya upande wa serikali na ule wa utetezi.
Washtakiwa Mrita na mwenzake Muyela waliachiwa huru mapema mwezi uliopita na kisha wakakamatwa tena na kusomewa upya Mashtaka ya mauaji.
Katika kesi hiyo, Washtakiwa hao wanatuhumiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya ambaye ni Dada wa bilionea Erasto Msuya.
Mauaji hayo yanadaiwa kutendeka huko Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.,Mei 25, mwaka jana.
Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Simba amesema Kuwa bado anafanya utafiti juu ya kesi hiyo."Maombi yaliyoletwa na upande wa utetezi na mjibu ya Jamuhuri, yanahitaji kifanyiwa utafiti wa kina kaba sijatoa uamuzi" amesema Hakimu Simba.
Kutokana na hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20 kwa ajili ya kutolewa Manji.
Awali mara baada washtakiwa kusomewa tuhuma zao za, mauaji, Wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliiomba Mahakama kufuta kesi hiyo akidai kuwa kuwa imefunguliwa kinyume na sheria kwani ilishafutwa.
Alidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kinyume na sheria kwa sababu ilishatolewa uamuzi Februari 23, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa ambapo aliwaachia huru washitakiwa wote.
"Maneno aliyoyatumia Hakimu katika uamuzi wake ni amewa-set free washitakiwa na si kuwa-discharge, hivyo hawa washitakiwa wapo huru na hawakupaswa kukamatwa na kuletwa mahakamani kusomewa kosa hilo la mauaji," alidai Kibatala.
Aidha alidai kuwa Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kulipokea jalada hilo na kuwasomea washitakiwa mashtaka yao kwa kuwa limeshatolewa uamuzi.
Akijibu hoja hizo Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi amedai kuwa washitakiwa wamesomewa kosa hilo kwa mujibu wa sheria.
Amedai kuwa uamuzi uliotolewa ulikuwa ni kuwafutia mashitaka ambapo Jamhuri ina uwezo wa kuwakamata tena washitakiwa na kuwasomea kosa hilo la mauaji.
Amebainisha kuwa haoni sehemu yeyote ambayo inaonesha kosa walilosomewa washitakiwa lipo kimakosa mahakamani hapo.
No comments:
Post a Comment