Habari : Waziri, Mwakyembe Apokelewa Ofisini kwake Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 29 March 2017

Habari : Waziri, Mwakyembe Apokelewa Ofisini kwake Dodoma




Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante ole Gabriel akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na wakati waziri huyo alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.





Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa Taaisi zilizo chini ya Wizara yake wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini za Wizara Mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(kushoto) akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) kuzungumza na waandishi wa habari Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mikakati yake katika kuiongoza Wizara.


Baadhi ya wakurugenzi wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao alipowasilikatika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.


Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

No comments:

Post a Comment