Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.
Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili.
Mmoja wa viongozi wa timu hiyo (kushoto), akitoa maelekezo kabla ya kuondoka uwanjani hapo. (Picha na blog ya habari za jamii.com)
Wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye gari kuelekea hotelini walikofikia.
Na Dotto Mwaibale
KIKOSI cha Timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga katika dimba litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imewasili leo (Alhamisi) saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.
Mara baada ya kuwasili timu hiyo ilipokelewa na wananchi wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini hata hivyo viongozi wa timu hiyo hawakuwa tayari kuzungumza chochote na wanahabari badala yake walipiga picha ya pamoja na wachezaji na kisha kupanda kwenye magari na kuondoka.
Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini humo Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kuwa waamuzi wake wanatarajiwa kufika kesho.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment