Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza amewaonya watumishi wa serikali ambao wanakwepa kushiriki mazoezi ya pamoja katika uwanja wa Samora na kuwa kuanzia sasa mtumishi atakayekwepa kushiriki kubanwa.
Alisema pamoja na kuwa mazoezi hayo ni kwa ajili ya afya za kila mmoja kujikinga na maradhi yanayosababishwa na kutofanya mazoezi ila bado mazoezi hiyo ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais kwa kila mtanzania.
Hivyo alisema kutokana na baadhi ya watumishi hasa wanawake kukwepa mazoezi hayo anaandaa mkakati wa kuwabana watumishi wote wanaokwepa mazoezi kwa kuitisha mazoezi siku ya kazi ili wale ambao watashindwa kufika watawajibishwa .
"Naangalia ni siku gani ambayo itakuwa ni siku ya kazi kama ijumaa ama siku nyingine yeyote ambayo nitaitisha mazoezi kuanzia ofisi yangu hadi Samora kwa kila mtumishi kushiriki na siku hiyo hata ofisini watumishi wakichelewa ni sawa lengo kuweza kufanya mazoezi na kutekeleza agizo la serikali ......nashangazwa sana awali wanawake ndio ambao walikuwa wakifika kwa wingi mazoezini ila leo hii idadi ya wanawake imepungua ukilinganisha na wanaume ....nawashangaa sana wanawake wanaokwepa mazoezi wakati ndio ambao wanakula vitu vyenye mafuta "
Hivyo alisema kuanza sasa kila mtumishi wa serikali lazima kufika katika mazoezi na utawekwa utaratibu wa kuorodhesha majina kila idara ya watu wanaoshiriki mazoezi .
Mkuu wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza (wa tatu kushoto) akiongoza mazoezi ya viungo katika uwanja wa samora Leo wa pili kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa wamoja Ayubu
DC Iringa Richard Kasesela wa kwanza kulia akishiriki mazoezi ya riadha kutoka uwanja wa Samora
Washiriki wa mazoezi wakiwasili ufisi ya RC Iringa wakitokea uwanja wa Samora
Afisa michezo mkoa wa Iringa Kenedy Komba akiorodhesha majina ya wakuu wa Idara walioshiriki mazoezi leo ni kuwabana wamnaokwepa mazoezi
Wanamazoezi wakitoka uwanja wa samora
Mkazi wa Iringa akiwa amebeba pombe aina ya komoni asubuhi ya leo pombe hii inatengenezwa kwa mahindi jambo ambalo serikali ya mkoa imepigamarufuku matumizi mabaya ya chakula
Mkazi wa Iringa akipishana na washiriki wa mazoezi huku akiwa amebeba pombe ya komoni inayotengenezwa kwa mahindi
RAS Iringa na RC Masenza kulia wakiwa katika mazoezi
RC Iringa Amina Masenza kulia akiongoza mazoezi saa 12 asubuhi ya leo
Afisa habari Manispaa ya Iringa Sima Bingilengi kushoto akiwajibika
Mwanahabari Manispaa ya Iringa Janeth Matondo kulia pia akishiriki mazoezi
DC Kasesela katikati wa pili kulia akiwa na wadau wa kwanza kulia ni Geofrey Mungai
Mzee Vitus Mushi akiwajibika mazoezini
DC Iringa Richard Kasesela wa tatu katikati kulia akiwa na mkurugenzi Manispaa ya Iringa Dr Wiliam na mwanasheria wa Iringa wa pili kulia
No comments:
Post a Comment