Matukio : DC Shinyanga Afungua Warsha ya Asasi za Kiraia - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Feb 2017

Matukio : DC Shinyanga Afungua Warsha ya Asasi za Kiraia


Ijumaa Februari 24,2017 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imezikutanisha Asasi za Kiraia zilizopo katika manispaa hiyo kwenye semina ya siku moja iliyolenga kuzijengea uwezo ili ziweze kutekeleza vyema shughuli zao katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Mgeni rasmi katika semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika manispaa ya Shinyanga alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.


Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo Matiro amezitaka asasi za kiraia (NGO’s,CBO’) kuepuka kuwa sehemu ya kushiriki uovu katika jamii wakitumia mwamvuli wa asasi na kuzitaka kuepuka kuilaumu serikali badala ya kuishauri pale inapokosea.


“Serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kiraia katika kuisaidia jamii,nyinyi ni sehemu ya serikali,mnafanya kazi pamoja na serikali kuisaidia serikali,serikali yetu haiwezi kufanya kila kitu,hivyo haipendezi kuilaumu serikali,ishaurini pale mnapoona mambo hayaendi sawa”,amesema Matiro.


“Pia msiwe na usiri katika shughuli zenu maana zipo asasi zinaingia kimya kimya katika jamii,kabla ya kuanza kutekeleza mradi jitambulishe katika jamii,elezeni mnafanya nini pia itatusaidia kujua asasi ipi inafanya nini hali ambayo itawezesha kupungua kwa idadi ya asasi zinazofanya shughuli moja katika eneo moja”, ameongeza Matiro.


Naye Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi amesema asasi za kiraia zinatakiwa kuwajibika kwa serikali hivyo zinatakiwa kuwa zinatoa taarifa serikalini kuhusu shughuli wanazofanya.


Miongoni mwa mada zilizotolewa katika semina hiyo ni pamoja na sheria za uendeshaji wa asasi za kiraia,taratibu za uendeshaji wa asasi za kiraia,namna ya kuandaa andiko la mradi na masuala yanayohusu rushwa.

Mwenyekiti wa semina hiyo Mchungaji Dkt. Meshack Kulwa kutoka TCCIA Shinyanga akimkaribisha mgeni,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili afungua semina hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo ambapo alisema serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kiraia na ipo tayari kushirikiano na asasi yoyote katika kuwaletea maendeleo wananchi

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini.Kulia ni Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo ukumbini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa asasi za kiraia katika manispaa ya Shinyanga

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza ukumbini.Kulia ni Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi akizungumza katika semina hiyo ambayo imekutanisha viongozi mbalimbali wa asasi za kiraia katika manispaa hiyo

Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi akisisitiza asasi za kiraia kushirikiana na serikali katika kuiletea maendeleo jamii

Afisa Uchunguzi Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga Alice Mazoko akitoa mada kuhusu masuala ya rushwa ambapo alizitaka asasi hizo kujikita katika malengo yao badala ya kugeuka kichochoro cha kuchuma pesa zisizokuwa halali (rushwa).

Afisa Uchunguzi Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga Alice Mazoko akisisitiza juu ya umuhimu wa asasi za kiraia kuepuka vitendo vya rushwa katika shughuli zao.

Lubumba Masebu kutoka asasi ya vijana ya Youth Development Organisation (YUDEN) akichangia hoja wakati wa semina hiyo ambapo alisema asasi nyingi hazifanikiwi kutokana na jamii kukosa elimu na kushindwa kuelewa malengo ya miradi husika

Mchumi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Mpasa akitoa mada kuhusu namna ya kuandaa andiko la mradi

Mchumi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Mpasa akiendelea kutoa mada.Kulia ni katibu wa chama cha watu wenye ualbino Lazaro Nael akimsaidia mawasiliano kwa njia ya ishara mmoja wa washiriki mwenye ulemavu wa kusikia (asiyesikia)

Mwezeshaji akitoa mada ukumbini

Washiriki wakiwa ukumbini

Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini….

Semina inaendelea

Washiriki wakiwa ukumbini

Semina inaendelea

Semina inaendelea

Viongozi wa asasi za kiraia wakiwa ukumbini

Mwezeshaji akitoa mada kuhusu sheria za uendeshaji wa asasi za kiraia

Afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Salome Komba akitoa mada kuhusu taratibu za uendeshaji wa asasi za kiraia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad