Maisha : Kinana Atembelea na Kuwafariji Yatima katika Kijiji cha Matumaini, Kisasa - Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


5 Feb 2017

Maisha : Kinana Atembelea na Kuwafariji Yatima katika Kijiji cha Matumaini, Kisasa - DodomaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto wa Kijiji cha Matumaini, kilichopo eneo la Kisasa Dodoma mjini alipotembelea kituo hicho kuwafariki watoto yatima, leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, ambayo kilele chake ni kesho. Kushoto ni mwanzilishi wa Kijiji hicho Padre Vincent Boseil

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Matumaini, kilichopo eneo la Kisasa Dodoma mjini alipotembelea kituo hicho kuwafariki watoto yatima, leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, ambayo kilele chake ni kesho. Kulia ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hicho Sista Roselie.Kinana akionyeshwa eneo ambako hutunza watoto wachanga, ambao ni yatima, kwenye Kijiji hicho cha Matumaini


Kinana akimchukua mtoto mmoja kumfurahia, katika eneo hilo la kulea watoto wachanga

Kinana akikaribishwa ndani na Mwanzilishi wa Kituo hicho, Padre Vincent Boseili

Kinana akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye kituo hicho cha Kijiji cha Matumaini

Padre Vincenti akionyesha wageni ramani ya Kijiji hicho cha Matumaini

Sista Roselie akisoma risala

Padre Vincent akitoa maelezo kuhusu kijiji hicho cha Matumaini

Waziri Mavunde akizungumza alipokaribisha kuongea kwenye kijiji hicho cha Matumaini

Mavunde akizungumzaMavunde akipongezwa na Kinana baada ya kuzungumza neno la shukrani kwa mwanzilishi wa Kijiji hicho chenye kituo cha watoto yatima

Kinana akimpongeza Padre Vincent baada ya kuzungumza maneno ya shukrani

Kinana na ugeni wake wakienda kukagua sguhuli mbalimbali kwenye Kijiji hicho cha Matumaini

Kinana akiwasalimia watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho ambao pia wanasoma

Kinana akiwasalimia wanafunzi wa Sekondari wanalelewa na kusomeshwa na Kijiji hicho cha Matumaini. Kushoto ni Padre Vincent wa Kijiji hicho

Watoto ambao ni wanafunzi wanaolelewa na kusomeshwa kwenye Kijiji hicho wakiimba wimbo wa Taifa Kinana alipowasili

Wanafunzi wa Kijiji hicho wakipiga ala wakati wimbo wa Taifa la Tanzania ukiimbwa

Kinana akifurahia jambo kwa kupiga kofi huku mtoto wa Kijiji hicho aliyempakata naye akipiga kofi

Wanafunzi wa Sekondari wanaolelewa na kusomeshwa na Kijiji hicho cha Matumaini wakiimba wimbo wao maalum

Kinana akiwafurahia wanafunzi ambao alitambulishwa kwao na Padre Vincent

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimfurahia mtoto anayelelewa katika Kijiji hicho cha Matumaini

Kinana akikabidhi zawadi kwa watoto

Kinana akifurahia watoto wa Kijiji hicho baada ya kuwapa zawadi

Kinana akishiriki kuimba wimbo maalum pamoja na wanafunzi wanaolelewa na kusomeshwa katika Kijiji hicho

Kinana akionyeshwa eneo ambako kinamama hujifungulia bure kwenye Kijiji hicho cha Matumaini

Kinana akizungumzana wageni kutoka Italia ambao nao walifika kutembelea Kijiji hicho cha Matumaini

Kisha Kinana akamchumu mtoto huyo kwa upendo mkubwa

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini akimchukua mtoto kwa upendo

Watoto katika Kijiji hicho wakitazama kwa mshangao ugeni wa Kinana

Katibu Mkuu Kinana akipewa maelezo kwenye mapokezi ya Hospitali ya Kijiji hicho cha Matumaini

Kinana akionyeshwa vifaa vya kupimia CD4 kwa wagonjwa wa Ukimwi

Kinana akimshukuru Padre Vincent baada ya kutembelea Kijiji hicho cha Matumaini

Kinana akiagana na Padre Vincnt kabla ya kuondoka

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini akiagana na Padre Vince pia kabla ya kuondoka. Picha zote na Bashir Nkoromo. KINANA ASHIRIKI NA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO DODOMA LEO IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO MIAKA 40 YA CCM

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Dodoma mjini na mkoa huo, katika Ofisi ya CCM mkoa wa Dodoma, leo alipowasili kwenye ofisi hiyo, tayari kushiriki na kukagua shughuli za maendeleo ikiwa ni sehemu ya Madhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho. Akizungumza Kinana amesema, CCM imeamua kufanya Maadhimisho hayo mkoani Dodoma kwa kuwa imedhamiriwa kuisaidia Serikali katika kutekeleza ilani ya CCM, hivyo CCM imeamua kufanya hivyo ili kuunga mkono azma ya Serikali kuhamia Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akitoa salamu za shukrani, baada ya Kinana kuzungumza katika mkutano huo wa ndani. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Adam Kimbisa.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasalimia mafundi alipowasili kukagua na kupanda miti kwenye mradi wa Ujenzi wa Dampo la Kisasa katika eneo la Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini, leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda miti kwenye mradi wa Ujenzi wa Dampo la Kisasa katika eneo la Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini, leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho.

Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Dodoma Mjini, akishiriki kupanda mji kwenye mradi huo

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini akishiriki kupanda mti kwenye eneo la mradi huo

Mbunge wa Dodoma Mjini, Waziri Anthony Mavunde akishiriki kupanda mti katika eneo hilo

Kinana akimpongeza kwa kupanda mti katika eneo hilo, Mzee Godfrey James

Kinana akimsaidia kupanda mti mjumbe wa shina katika kata hiyo Ester Paschal

Kinana na ujumbe wake wakiondoka katika upandaji mti na kwenda kukagua ujenzi wa dampo la kisasa katika eneo hilo. Kushoto ni Mavunde na kulia ni Kimbisa

Mhandisi wa Manispaa ya Dodoma, Injinia John Nchilla akimpa Kinana maelezo kuhusu ujenzi wa dampo hilo la Kisasa katika Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini

Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Nkuhungu, Dodoma Mjini, Pius Afa akimkaribisha Kinana kushiriki ujnezi na kupanda mti kwenye ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata hiyo

Wanachi wakimpokea Kinana kwa shamrashamra alipowasili katika Kata hiyo ya Nkuhungu

Kinana akisalimia wananchi wa Nkuhungu

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nkuhungu Pius Afa akimuonyesha Kinana ramani ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM ya Kata hiyo

Kinana akipokea tofali alipokuwa akishiriki ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM Kata ya Nkuhungu

Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Nkuhungu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40ya CCM ambayo kilele chake ni kesho

Kinana akishuka baada ya kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo kikamilifu
Kinana akizungumza na wananchi baada ya kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Mkuhungu, Dodoma leo. Picha zaidi alipotembelea Kijiji cha Matumaini

Post Top Ad