Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu kwani ni urithi wa kila mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huu wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.
Rais Msataafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akizungumza mara baada ya kupokea Matembezi kwa ajili ya kupinga ujangili ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 Jumamosi jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yameratibiwa na Asasi ya Tanzania – China Promotion Association (TCFPA) na Ubolozi wa China ambapo yalianzia Ofisi za Ubalozi wa China na kuishia katika Hotel ya Sea Cliff.
Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing, akizungumza kabla ya kuanza matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 Jumamosi jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yana lengo la kuhamasisha upingaji wa ujangili na mauaji ya Tembo.
Katibu Mkuu wa Asasi ya Tanzania – China Promotion Association (TCFPA) akitoa maelekezo kuhusu matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 Jumamosi jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yameratibiwa na asasi hiyo kwa kushirikiana na Ubolozi wa China ambapo yalianzia Ofisi za Ubalozi wa China na kuishia katika Hotel ya Sea Cliff.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi (kushoto) akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 yaliyofanyika Jumamosi jijini Dar es Salaam. Lengo la matembezi hayo ni kuhamasisha jamii kupinga ujangili na mauaji ya Tembo.
Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing, akiwaongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kufanya mazoezi kabla ya kuanza matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 Jumamosi jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yana lengo la kuhamasisha upingaji wa ujangili na mauaji ya Tembo.
Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing (mwenye tisheti nyekundu), akiwaongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 Jumamosi jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi na kulia kwa Balozi ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi.
Baadhi ya washiriki wa matembezi ya Walkt for Elephant Dar es Salaam 2017 wakiwa wakionyesha umoja wao katika kupinga mauaji ya Tembo mara baada ya kufika katika viwanja vya Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Jumamosi
Wanamuziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro wakiimba wimbo wenye ujumbe kuhusumauaji ya Tembo mbele ya Rais Mstaafu Benjamini Mkapa wakati wa hafla ya matembezi ya Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 yaliyofanyika jana Jumamosi. Picha zote na Frank Shija – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment