Matukio : Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ashiriki ibada ya Mwaka Mpya ,Monduli Arusha - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Jan 2017

Matukio : Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ashiriki ibada ya Mwaka Mpya ,Monduli ArushaWaziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa KamatiKuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017 ambapo amewataka watanzania wote bila kujali itikadi zao kufanya kazi kwa bidii.

Mh Lowassa ameshiriki ibada hiyo akiambatana na familia yake pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali Mkoani Arusha na Jimbo la Monduli wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mh Isack Joseph , Wakili John Mallya na viongozi wengine.

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa, mama Regina Lowassa akisalimiana na mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha Laison Saning'o katika Ibada maalamu ya mwaka mpya 2017.

+
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akisalimiana na mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha Laison Saning'o katika Ibada maalamu ya mwaka mpya 2017.

Wakili John Mallya (aliyeshika biblia) akisoma neno kwenye biblia katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017.

Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.

Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.

Post Top Ad