Meli Kubwa inayoweza kuingia abiria 1600, magari 50 na mizigo kwa pamoja ambayo itafanya safari zake kati ya Tanga-Unguja na Pemba ikiwa inaingia bandari ya Tanga leo wakati wa uzinduzi wake ambapo uwekezaji huo mkubwa umefanywa na kampuni ya Azam Marine ili kuwanusuru wananchi wa mkoa wa Tanga na changamoto za usafiri huo
Meli Kubwa inayoweza kuingia abiria 1600 na magari hamsini yenye mizigo kwa pamoja ambayo itafanya safari zake kati ya Tanga-Unguja na Pemba ikiwa inaingia bandari ya Tanga leo wakati wa uzinduzi wake ambapo uwekezaji huo mkubwa umefanywa na kampuni ya Azam Marine
Meneja Mkuu wa Azam Marine Hussein Mohammed wa pili kulia akitazama namna wananchi wanavyoshuka kwenye meli hiyo itakayopunguza adha na usumbufu kwa wananchi wanaosafiri kutoka mkoani Tanga kwenda Unguja na Pemba
Meneja Mkuu wa Azam Marine Hussein Mohammed katikati akizungumza na watumishi wa mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga wakati wa ujio wa meli hiyo kwenye bandari ya Tanga kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Tryphoni Ntipi kushoto ni PRO wa Mamlaka hiyo,Moni Jarufu.
Meneja Mkuu wa Azam Marine Hussein Mohammed katikati akisalimiana na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Tryphoni Ntipi wakati wa ujio wa meli hiyo kushoto ni PRO wa Mamlaka hiyo Bi. Moni Jarufu.
Mazungumzo yakiendelea
Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa meli hiyo kulia Mkurugenzi Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini (SUMATRA) Kaptain Mussa Mandia
Mkurugenzi Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini (SUMATRA) Kaptain Mussa Mandia katikati akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed
Nahodha wa Meli hiyo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika Bandari ya Tanga.
Waandishi wa Habari wakiwa kazini kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania katikati ni Mariam Shedafa wa Azam TV
Vifaa vya uokozi wakati wa majanga ya ajali hivyo
Baadhi ya Sehemu ya VIP ndani ya Meli hiyo kama inavyo onekana
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment