Makala /Muziki : Nyimbo 20 Nilizozipenda zaidi kutoka Tanzania 2016 - Jeff Msangi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Jan 2017

Makala /Muziki : Nyimbo 20 Nilizozipenda zaidi kutoka Tanzania 2016 - Jeff Msangi




Na Jeff Msangi , Canada

 
Mwaka 2017 ndio kwanza umeanza. Bado tuna matongotongo ya 2016. Sufuria kubwa la pilau la sikukuu bado limelowekwa. Mapambo ya Mas Mas yangali yakiwaka kwenye mti na ukutani. Ohh 2016. Ulikuwa na mengi weye. Tafakuri mbalimbali zinaendelea huku mipango ya 2017 imeshaanza kutekelezwa. Dunia na saa zake inasonga.

Ulipotoka panaweza kuwa muhimu sawa na unapokwenda. Historia,wanasema wahenga, ni Mwalimu wa kutosha. Tunapoianza 2017 sio vibaya kuangalia 2016 hata kama ni kwa kutumia side-mirror. Kama unavyoiacha Milima ya Kitonga, 2016 nayo unaiona ileee. Tunataka tujue wapi tulijikwaa na wapi tuliangukia. Ukijikwaa kwenye kichuguu ni ngumu kuangukia kwenye kichuguu.

Kwenye sanaa yalijiri mengi. Vijana walichuana katika kutuletea burudani. Ni jambo la kheri. Sanaa huweka vyema historia ya jamii. Zaonya,kuelekeza na kufunza achilia mbali kuburudisha.Kazi nyingi zilikuwa nzuri. Rafiki yangu,ndugu yangu Brian huwa anapenda kuipa kazi ya sanaa muda. Anasema ikidumu kwa muda fulani basi hiyo kazi ni nzuri. Imestahimili jaribio la muda.

Huku nikijaribu kuzipa muda, kati ya nyimbo nyingi zilizotoka nchini Tanzania katika mwaka 2016, Top 20 zangu ni hizi hapa chini. Kwa sababu mbalimbali nilizipenda.Yaweza kuwa mdundo na maneno. Mimi huheshimu sana utunzi. Nasikiliza neno kwa neno. Rafiki yangu, Fadhy Mtanga, naye ni mgonjwa wa nahau na misamiati.

Sasa ukihesabu utaona zipo 21 badala ya 20. Sababu ni kwamba wimbo wa mwisho kwenye orodha wa Chura, ulifungiwa na kisha kufunguliwa. Hata hivyo uliibua hisia nyingi. Sanaa na hadhira.Ujumbe ulifika. Msamiati ukatufikia.

Kisha kuna nyimbo ambazo nimeziweka kwenye Bonus. Sababu ni kwamba pamoja na ukali wake, hazikupata nafasi ya kuziteka nyoyo za watu hususani kitaa.Ndio maana utakuta kwenye orodha kuna nyimbo zina views za hatari kwenye YouTube nk ilhali zingine zina views za kawaida tu lakini zimo kwenye orodha. Mtaani zilikamata zaidi. Na zingine (kama kwenye Bonus) zipo mbioni kukamata pia kitaa. It takes time.

Pamoja na utashi wangu binafsi, nilishirikisha watu kadhaa wadau wa masuala ya burudani kupata insight za mambo fulani fulani. Shukrani kwa wadau kama Suka,MX,Chris Kaoneka nk. Suka umetisha sana mzazi.

Pamoja na jitihada zote,bila shaka kuna nyimbo kali ambazo nimezipisha. Niwie radhi.Kupitia sehemu ya maoni au email,tuwasiliane. Niambie kwanini unadhani wimbo fulani ulistahili kuwemo.

** Mpangilio hauna maana yoyote maalumu.
KWA NYIMBO ZINGINE ZAIDI BOFYA HAPA Bongo Celebrity...

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad