Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis akiongea na wajumbe wa baraza hilo katika kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro,Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Caroline Augustino.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa na kuwapongeza kwa kazi wanazoendelea kuzifanya kwa maslahi ya watoto nchini Leo Mjini Morogoro, Kulia ni Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa ambapo aliwataka katika agenda zao wajadili ukatili dhidi ya ubakaji na ushoga na hatimaye wampelekee taarifa ili kujua nini serikali ikifanye, Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Mkoa wa Dodoma Helena Charles.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa Komputa Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Mkoa wa Lindi Juma Adinani. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto kutoka Kinondoni Caroline Augustino. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Temeke Rehema Miraji. . Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mwenyekiti wa Baraza la Watoto kutoka Zanzibar Ameir Haji Khamis. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa kompyuta Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Mkoa wa Mwanza Apwiyamwene Nicholaus.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mjumbe wa Baraza la Watoto kutoka mkoa wa Singida Elibariki Abraham.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufungua kikao kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na walezi wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufungua kikao kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara hiyo (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) baada ya kufungua kikao kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro. PICHA NA HASSAN SILAYO-IDARA YA HABARI (TIS)
Na Anthony Ishengoma-MCDGC
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha Dawati la Ulinzi la na Usalama katika shule zote pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi ya Kata na Vijiji Nchini kote ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema hayo wakati akiongea katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu cha Baraza la Watoto la Taifa kinachofanyika kwa siku mbili Mjini Morogoro.
Aidha amewataka wajumbe wa Kikao hicho kujadiliana kwa kina juu ya ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na kuwasilisha mapendekezo yao Wizarani akisema kuwa hivi karibuni vitendo hivyo vimeongezeka kwa wingi sana katika Jamii.
Aliongeza kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa Mpango Mkakati wa Kupambana na Kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa miaka mitano Serikali itahakikisha vitendo vya ukatili vinapunguzwa kwa asilimia hamsini kupitia mpango kazi huo na kuongeza kuwa vitendo vya ukatili kwasasa vinatofautiana viwango akitaja ukatili huo kuwa ni ubakaji, ulawiti, ukeketeji, mimba na ndoa za utotoni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Caroline Augustino akiongea na vyombo vya Habari baada ya ufunguzi huo kuwa pamoja na kukutana leo jijini Morogoro pia Baraza hilo limefanya ziara mbalimbali mikoani kwa lengo la kuandaa makala maalumu za uelimishaji jamii kwa njia ya radio na runinga ili jamii iweze kufahamu maana na aina za ukatili dhidi ya watoto.
Adha Bi. Carolini amewataka wasichana walio katika umri mdogo kuachana na tamaa zinazowapelekea kujiingiza katika matendo mabaya yanayosababisha kukatisha ndoto zao ikiwemo kushindwa kuendelea na masomo pamoja na kujikuta wanapata ndoa za utotoni na kuwataka wazazi na walezi kutambua kuwa mtoto wa kike ana fursa sawa na watoto wakiume hasa kwa jamii za vijiini.
Bi. Caroline pia amezitaka jamii za wafugaji na badhi zilizoko kanda ya ziwa kuacha tabia ya tohara mbili kwa watoto wa kiume na tohara kwa watoto wa kike akisema tohara kwa wanawake inasababisha vifo na maumivu ambayo huleta hathari mbaya kwa wanawake kwa kipindi kirefu.
Kakao cha Baraza Kuu la Watoto Taifa pamoja na mambo mengine kinakutana kujadili kuandaa Mkutano Mkuu wa Baraza la Watoto Taifa utakaofanyika Mwezi Aprili Mwaka huu.
No comments:
Post a Comment