MKURUGENZI Mtendaji wa Jamii Media na mwanzilishi wa mtandao maarufu wa JamiiForums na Fikra Pevu,Maxence Melo.
Ndugu Maxence Melo amepatiwa dhamana kwa makosa yake anayoshtakiwa likiwemo la kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa na Serikali.
Anakabiliwa na Mashtaka Matatu likiwemo la kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa nchini au haina domain ya Tanzania (.co.tz) kinyume cha kifungu cha 7 cha sheria ya EPOCA.
Mashtaka mengine ni kuzuia na kuharibu data ambazo jeshi la polisi wamekuwa wakitaka kwa ajili ya uchaguzi chini ya kifungu cha 22 cha Cyber Act.
Pia ,kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu 22 cha Cyber Crime.