Matukio : Waziri Mkuu, Majaliwa awasili Loliondo kuendelea na ziara ya Mkoa wa Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Dec 2016

Matukio : Waziri Mkuu, Majaliwa awasili Loliondo kuendelea na ziara ya Mkoa wa Arusha



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kiltaro katika tararafa ya Loliondo kuendelea na ziara yake wilayani Ngorongoro Desemba, 15, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake wa Kimasai wakati alipotembelea Kituo mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni kilichojengwa na UNICEF katika kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi mbalimbali za mikono hasa mapambo yanayotengenezwa na wanawake wa kimasai katika kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wakati alipotembelea Kituo cha Mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni kijijini hapo Desemba 15, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la Emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016.

Wananchi wa kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasalimia akiwa ktika ziara ya wilaya ya Ngorongoro Desemba 15, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanchi wa kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Post Top Ad