Habari : Benki ya NMB Yadhamini Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Desemba 5 - 6, 2016 - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Dec 2016

Habari : Benki ya NMB Yadhamini Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Desemba 5 - 6, 2016Akizungumza  mbele ya Wanahabari  mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Sanaa,Michezo  na Utamaduni ,Mh Nape Mosses Nnauye,

"Mgeni rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni  Waziri Nape Nnauye,lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo  juu ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili  na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.

Alisema kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya  ya mitandao hii,

 Mkutano huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akizungumzia udhamini wa benki ya NMB katika mkutano mkuu wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili na kuwakutanisha blogger kutoka Tanzania Bara na Visiwani.   
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi(wa pili kutoka kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale kwa ajili y kudhamini mkutano huo Chama cha Bloggers Tanzania (TBN).

Post Top Ad