#FreeMaxenceMelo : Wakili wa Jamii Forums anasema mteja wake anakomolewa - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Dec 2016

#FreeMaxenceMelo : Wakili wa Jamii Forums anasema mteja wake anakomolewaMaxence Melo, muasisi wa Jamii ForumsWakili Benedict Ishamakaki anayemwakilisha mahakamani mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media ya nchini Tanzania, kampuni inayomiliki mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo alisema mtazamo anaouona katika kesi ya mteja wake ni kama anakomolewa.

Alipozungumza na Sauti ya Amerika-VOA inayotangaza kutoka Washington DC, mwanasheria Ishamakaki alisema ukiangalia chombo kilichomfungulia mashtaka mteja wake, katika barua kutoka kwenye chombo hicho waliandika walikuwa wanasumbuka kumuandikia barua Melo ili kupata taarifa Fulani, kwa maana hiyo kwa maoni yake mwanasheria anaona kama ni “kulipizana kisasi kwamba wewe ulikuwa unatusumbua kupata taarifa ngoja na sisi tukusumbue kupata dhamana”.

Pia aliongeza kuwa mazingira yaliyotengenezwa mahakamani siku ya Ijumaa aliposomewa mashtaka na kupelekea mteja wake kukosa dhamana kwa maoni yake anaona kama “wanachezewa mchezo Fulani”.Mahojiano ya VOA na wakili Benedict Ishamakaki
Source : VOA Swahili

Post Top Ad