Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA , Geoffrey Sabuni akizungumza katika mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha VETA, Chang’ombe, Douglas Kipokola akitoa maelezo katika mahafali ya 46 ya chuo hicho leo jijni Dar es Salaam.
Wahitimu wakiimba shairi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu wakati wa Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA , Geoffrey Sabuni akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
NCHI inakwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo vinahitaji wataalam mbalimbali katika kuweza kufikia uchumi huo kwa kuhitaji wataalam wanaozalishwa nchini wakiwemo wahitimu wa mafunzo stadi yanayotolewa na vyuo vya VETA.
Hayo ameyasema leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), Geoffrey Sabuni wakati wa mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA, Changombe Dar es Salaam, amesema VETA inazalisha wataalam ambao wamebobea kwa ujuzi.
Amesema wahitimu wa VETA hawatafuti ajira kutokana na kuwa ujuzi wanaoupata unawawezesha kujiajiri au kuajiriwa kwa kutafutwa na wamekuwa wakifanya vizuri katika maeneo walioajiriwa na kujiajiri.
Sabuni amesema wanaosoma VETA wapo waliohitimu kidato nne hadi waliopata shahada ya kwanza hivyo jamii iondoe dhana ya kwamba wanaosoma VETA ni wale walioshindwa kufanya vizuri katika shule za sekondari na msingi.
Aidha amewataka wahitimu wanaozalishwa na vyuo hivyo kuwa na weledi katika kufanya kazi na kuondokana kuwaibia waajiri hali ambayo itafanya baadhi yao kupoteza sifa ya kujiajiri au kuajiliwa.
Nae Mkuu wa Chuo cha VETA Changombe, Douglas Kipokola amesema kuwa wahitimu mwaka huu wako 423 katika fani mbalimbali na kwamba wapo tayari katika soko la ajira kutokana na mafunzo walioyapata.
Amesema kuna changamoto za walimu ambapo wameshaanza kulifanyia kazi kutokana na mitaala inahitaji mafunzo yenye tija kwa uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi wasiozidi 20.
No comments:
Post a Comment