Na Dixon Busagaga.
SHRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeanza jitihada kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Mashirika makubwa ya ndege ,kuona ni namna gani yanaweza kusaidia katika
kuinua sekta ya utalii hapa nchini.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi na
Hifadhi za taifa ,ndege aina ya ATR namba 5H-PWE inatua katika uwanja wa ndege
uliopo katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti huku ikiwa na abiria 45 kutoka
nchini Afrika kusini waliofika kwa ajili ya Utalii.
Ndege hii mali ya kampuni ya Shirika la ndege la
Precision Air imetua majira ya saa 11:40 juzi jioni ikiwa ni ishara ya uzinuzi
rasmi wa safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi katika hifadhi ya
Serengeti ambazo sasa zitafanyika mara tatu kwa juma.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuanza kwa safari za ndege katika hifadhi hii
kutaongeza idadi ya watalii ambao kwa sasa watatumia muda mfupi kufika
hifadhini.
Kwa upande wa kampuni zinazojishughulisha na
biashara ya utalii nchini hatua ya shirika la ndege la Precision Air kufanya
safari za moja kwa moja hadi hifadhi ya Serengeti ina maana gani kwao.
Hatua hii ikalisukuma Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanapa ,sasa kuangalaia uwezekano wa kuendelea kutoa ushawishi kwa mashirika
mengine ya ndege kufanya safari zao katika hifadhi zilizopo kusini mwa Tanzania.
Kuhusu usalama katika viwanja vya ndege vilivyoko
katika Hifadhi za taifa Shelutete ameyaondoa hofu mashirika ya ndege na kwamba
viwanja vimekaguliwa na vina uwezo wa kupokea ndege mbalimbali.
Kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja hadi
katika hifadhi za taifa ni fursa nyingine kwa Tanapa na kampuni za Utalii
nchini kwa kuongeza idadi ya wageni watakaotembelea vivuito vya utalii na
kuongeza pato la taifa kupitia fedha za kigeni.
No comments:
Post a Comment