Usalama Barabarani : Wiki ya Nenda kwa Usalama Yazinduliwa Arusha / Dar es Salaam. - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Nov 2016

Usalama Barabarani : Wiki ya Nenda kwa Usalama Yazinduliwa Arusha / Dar es Salaam.


 Polisi wa kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam, akiongoza bajaj wakati wa maandaano ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga Novemba 7, 2016. Katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bw. Felix Lyavivaakimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Kikosicha usalama barabarani kilitumia wasaa huo kuwaelimisha wananchi, sheria mbalimbali zinazosimamia usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari kwa madereva wa vyombo vya moto, na matumizi ya alama za kuongoza magari pamoja. Wilaya zote tatu na zile mpya ziliwakilishwa na makamanda wa vikosivya usalama barabarani, wakiongozwa na wajumbe wa baraza lausalama barabarani la mkoa. Sambamba na hayo, palikuwepona burudani mbalimbali, wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man na Msaga Sumu ambaye wimbo wake unatumika kutangaza hatua za kuzngatia katika kuzingatia sheria za usalama barabarani, lakini pia walikuwepo wasanii wa jeshi la polisi na wale wanafunzi ktoka shule ya Jeshi la Wokovu. Uzinduzi huo ulitanguliwa na maanadamano ya waendesha bodaboda, bajaji, magari ya kawaida na yale ya mafunzo ya udereva.
  Polisi wa kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam, akiongoza maandamano  ya magari wakati yakiwasili viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam


 Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilayaya Temeke jijini Dar es Salaam, Bw. Felix Lyaviva akisalimiana na makamandawa polisi, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, viongozi wa dini na wajumbe wa baraza lausalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam.
 Bw. Lyaviva akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP, Gilles Mroto
 Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Aziz Varda
  Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Iddi Azan
   Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum
 Mkuu wa wilaya akisalimiana na Makuu wa Uhamiaji wilaya ya Temeke
 Mkuu wa Wilaya akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP, Salum Hamduni
 Mkuu wa wilaya akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kionondoni, ACP Theopista Malya
 Mkuu wa wilaya akisalimiana na Mkuu wa magereza


 Mkuu wa wilaya akisalimiana na Kamanda wa polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Temeke, (RTO), ASP, Solomon Mwangamilo.
 Polisi wa Usalama barabarani wakiwasili kwa maandamano
 Brass Band ya polisi ikiongoza maandamano
 Wanafuzni wa sekondari
 Meza kuu
 Maafisa wa polisi na wajumbe wa baraza la usalama barabarani
 Kwaya ya shule ikiongozwa na afisa wa polisi, ikihamasisha umuhimu wa kuzingatia sheria zausalama barabarani
 Msanii wa jeshi la polisi
 Kamanda wa polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Temeke, (RTO), ASP, Solomon Mwangamilo.
 Mkuu wa kituo cha polisi (OCS), stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo Bus Terminal, ASP, Sarah Bundala, akiwasikiliza vijanahawa ambao ni madereva wa bodaboda
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, MsagaSumu (kushoto) na Tunda Man, wakitumbuiza huku mlinzi wao (Bodyguard) akiwa nyuma
 Afisa wa polisi wa kikosi cha usalama barabarani Sophia, akiwaongoza wanafunzi
 Mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Iddi Azan, akiteta jambo na Kamanda Solomon


Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini,Henry Tzamburakis cheti cha kutambua mchango mkubwa wa udhamini unaotolewa na kampuni hiyo  katika kuadhimisha wiki ya  Usalama barabarani jijini Arusha.Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani wakitazama bidhaa za Vodacom katika  banda la Vodacom Tanzania kwenye wiki ya Usalama barabarabani inayoadhimishwa jijini Arusha.

Post Top Ad