Usalama Barabarani : Madereva Bodaboda wawalalamikia Askari wa usalama barabarani wanaotumia PikiPiki ( VodaFasta ), Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Nov 2016

Usalama Barabarani : Madereva Bodaboda wawalalamikia Askari wa usalama barabarani wanaotumia PikiPiki ( VodaFasta ), Arusha


Katibu tawala wa Wilaya   ya Arusha Arusha David Mwakiposa  akiwa anaongea na waendesha bodaboda wa  wilaya ya Arusha waendesha bodaboda wakiwa wanamsikiliza katibu tawala wa wilaya kwa makini (Hawapo pichani).


Na Woinde Shizza,Arusha



 Baadhi ya Vijana wa mkoa wa Arusha  wanaofanya kazi ya kuendesha bodaboda  wamelalamikia kitendo cha polisi wajulikanao kwa jina la Voda fasta kuwatoza rushwa kila kona  pamoja na jiji kutowapa mikopo ya Vikundi jambo ambalo wamedai linawanyima raha na uhuru wa kufanya kazi .



Hayo wameyasema leo wakati mkutano baina yao na katibu tawala wa Wilaya   ya Arusha Arusha David Mwakiposa wakati alipokutana nao kusikiliza kero zao zinazowakabili vijana hao ambao wanaendesha bodaboda



Mbali na kero hiyo pia wameilalamikia Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushindwa kuwapa mikopo ambayo inaweza kuwasaidia  kujiajiri wenyewe .



Mmoja wa vijana hao bodaboda ambae alijitambulisha kwa jina la Daudi Molel alisema kuwa wamekuwa wakipata kero sana haswa kutoka kwa hawa askari polisi wanaojulikana kwa jina la Vodafasta kwani wamekuwa wakiwakamata hovyo na wamekuwa wakiwatafutia makosa mengi ili mradi tu wapewe rushwa.



“unajua unakuta mimi nimeshusha abiria ghafla wanakuja anaanza kukutafutia makosa kibao ukikataa wanachomoa fungua wanaondoka nazo kitu ambacho sio kizuri kabisa na akiridhishi kabisa ,mimi nimeajiriwa tajiri amenituma fedha nahitaji kupitia hiii hii bodaboda yangu nilishe familia nivalishe sasa jamani wanavyotudai rushwa kila mahali wanapotukamata wanatuhumiza sana tunaomba serikali itusaidie kwa hili “Alisema Asea Akyooo



 Aidha aliongeza kuwa kwa upande wa jiji wamekuwa wanatoa fedha za mikopo kwa kificho sana  kwani wamekuwa wanatoa fedha hizo kwa upandeleo na wanachagua vijana wa kuwapa na wao kama maderea bodaboda wamesahaulika kabisa hivyo wanauomba uongozi usika wawafikirie  na wao ili waweze kupata mikopo  kwa ajili ya kujinunulia pikipiki zao binafsi na waweze kujiajiri.



Akijibu hoja hizo katibu tawala wa   wilaya ya Arusha David Makiposa aliwasihi vijana hao kuunda vikindi na serikali ya wilaya ya Arusha ipo tayari kuwasimamia  kuhakikisha nao wananufaika na pesa za mikopo ya jiji  na serikali imeshatoa maelekezo  kwa uongozi wa jiji kuhakikisha katika fedha watakazotoa kwa awamu hii wahakikishe kundi la boda boda   linapewa kipaumbele cha kipekee.



Alisema kuwa   dhamira ya dhati ya serikali  ni kutatua kero za wananchi  kwa haraka iwezekanavyo  ,hivyo azma ya serikali ya awamu ya tano  ni kila kiongozi ama mtendaji anatatakiwa kutatua kero  zilizopo  katika eneo lake ipasavyo ivyo hana  sababu ya kukaa ofsisini wakati kuna maelfu ya  wananchi  wanyonge wanateseka mtaani na wakiwa wanakabiliwa na  kero  mbalimbalimbali.



Pia  alitumia muda huo kuwashukuru  watendaji wa kata kwa akuanza kutatua kero za wandesha bodaboda hao  na kuwaagiza wengine kwenda kuweka program maalumu  za kukaa na bodaboda na kuwasaidia shida zao  na aliaidi kuendelea kuwafatilia.



Aidha  katika mambo ambayo kikao hicho kiliazimia ni pamoja na kuundwa  uongozi wa wilaya  kila kata ,kanda ya wilaya  ndani ya siku saba ili waendesha bodaboda wapate chombo cha kuwasemea matatizo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad