Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani |
Na Margareth Chambiri – Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani
amesema jambo kubwa ambalo watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na
Uchaguzi wa Marekani uliomalizika hivi karibuni ni kwa wananchi
kuheshimi mifumo ya Uchaguzi.
Mkurugenzi
Kailima ametoa kauli hiyo ikiwa ni tathimi yake kuhusu uchaguzi huo wa
Marekani na namna ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusu
ucheleweshaji wa kutangaza matokeo ya uchaguzi unaofanywa na Tume
ikilinganishwa na ilivyofanyika nchini Marekani.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na
Kituo cha Redio cha Clouds FM, Kailima amesema siyo sahihi kulinganisha
uchaguzi wa Marekani na Tanzania, akitolea mfano sekta ya mawasiliano
ambayo ni muhimu katika kusafirisha vifaa na taarifa mbalimbali za
uchaguzi inavyokabiliwa na changamoto.
Amesema
watanzania na hasa Wapiga kura wengi wanaishi maeneo ya vijijini ambayo
baadhi yake hayafikiki kwa urahisi na kwamba haiwezekani Tume
ikatangaza matokeo bila kuhakikisha kuwa kila kura imehesabiwa ikiwemo
ya yule mwananchi wa kijijini.
Amebainisha
kuwa yapo mambo ya msingi ambayo watanzania wanapaswa kujifunza
kutokana na Uchaguzi wa Marekani, kubwa ikiwa ni hatua ya kuheshimu
mifumo ya Uchaguzi sambamba na Mamlaka zinazosimamia chaguzi hizo.
Ametolea
mfano wa uvumilivu katika kusubiri matokeo na Wagombea kuheshimu
matokeo yanayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria
kwani hata pale ambapo anayeshindwa hakuridhika bado anaweza kupinga
matokeo kwa kufuata taratibu zilizopo kisheria.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inakamilisha Mwongozo wa Utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura wa 2015-2020 ili
iweze kuzishirikisha Asasi za Kiraia, Taasisi au Vikundi mbalimbali vya
Watu wanaotaka kutoa Elimu hiyo.
Kwa
mujibu wa Bwana Kailima Tume imo katika hatua za mwisho za kupitia
Rasimu ya Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura kwa ajili ya kuupitisha uweze
kutumiwa na Wadau mbalimbali wa Uchaguzi.
Amesema
pamoja na hatua ya Tume ya kuanza kutoa Elimu ya Mpiga Kura mapema
kuliko ilivyozoeleka na wananchi, inakusudia kupanua zaidi wigo wa
utoaji wa Elimu hiyo kwa kuwashirikisha wadau wengi zaidi wakiwemo
Viongozi wa Dini.
Bwana
Kailima amesema Tume kupitia kwa Mwenyekiti wake Mheshimiwa Jaji
(Mstaafu) Damiani Lubuva baadaye mwezi huu itatoa taarifa rasmi kwa
ajili ya kuzialika Taasisi na Asasi za Kiraia zinazotaka kutoa Elimu ya
Mpiga Kura kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya kupatiwa kibali rasmi cha
kutoa Elimu ya Mpiga Kura.
Aidha
Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amevitaja vigezo vya kupatiwa kibali kwa
ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuwa ni pamoja na Cheti cha Usajili,
Asasi au Taasisi kuwa imefanya kazi nchini kwa kipindi kisichopungua
miezi sita pamoja na kuwasilisha majina ya watendaji wa juu wa Taasisi
au Asasi husika.
Akizungumzia
kuhusu tathmini ya zoezi hilo linaloendelea kufanywa na Tume yake,
Bwana Kailima Halmashauri amesema limekuwa na mafanikio makubwa na
anaamini kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Uchaguzi kutawezesha
wananchi wengi kufikiwa na Elimu hiyo na kwamba Uchaguzi Mkuu wa Mwaka
2020 hakutakuwa na malalamiko na badala yake zoezi la uchaguzi litakuwa
rahisi.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi tayari imeanza utekelezaji wa zoezi la Utoaji wa
Elimu ya Mpiga Kura ambapo imeshiriki katika maonesho mbalimbali
yakiwemo ya Biashara ya Kimataifa na yale ya Wakulima pamoja na
kutembelea na kutoa Elimu ya Mpiga Kura katika shule kadhaa za Sekondari
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment